”Ninahakika Nyani ni ‘Smart’ Kuliko Wabaguzi wa Rangi”- Balotelli



Super Mario Balotelli ameonyesha kuunga mkono harakati za ‘Black Lives Matter’ baada ya kifo cha Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi nchini Marekani.

Mario Balotelli performed Black Power pose as he supported the Black Lives Matter protests

Wanaharakati wamekuwa wakitaka haki juu ya kifo hicho cha Floyd, ambaye alifikwa na umauti siku ya Jumatatu baada ya kukandamizwa na goti huku shingo yake ikiwa chini ya sakafu na askari polisi, Derek Chauvin.

Brescia forward Balotelli joined the likes of Paul Pogba in making a stand against racism

Maafisa wa majimbo wamechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwapeleka maelfu ya wanajeshi wa ulinzi wa taifa, kuweka amri za kutokuwa nje usiku na kufunga mifumo ya usafiri wa watu wengi ili kupunguza mavuguvugu ya maandamano, lakini hilo halikuzuia baadhi ya miji mingi kushuhudia vurugu.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Brescia, Balotelli amejiunga na mastaa wengine kutoka Manchester United kama vile Paul Pogba na Marcus Rashford katika kusimama kidete kupinga vitendo vya kibaguzi.

Akiwa katika pozi la ‘Black Power’, Balotelli ameandika ujumbe wake katika akaunti yake ya Instagram kuwa ”Sina chochote dhidi ya nyani, kwasababu ninahakika nyani yupo ‘smart’ zaidi ya wabaguzi wa rangi.”


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad