Nishauri: Mke Wangu Kanijibu Yeye ni Mrembo, Anatongozwa Kila Siku na Kunambia Maisha Anayaweza sio Lazima Kuwa na Mimi
0
June 18, 2020
Habari zenu wakuu.
Sio mara ya kwanza kuomba ushauri juu ya migogoro yangu Mimi na mwenzangu (mke) pia nimekuja kwenu kwa mara nyingine tena kwakua this time naona imekua too much na nimeona bora nijitoe kwenye mashindano.
Inshort aliyekua mke wangu nilianza nae mahusiano yapata miaka 6 mpaka sasa lakini ndoa yetu ina mwaka sasa na miezi 4 ni waajiriwa wote kwani tulipata kazi kwenye kampuni ya mawasiliano ila department tofauti
Kwenye kazi sasa tuna miaka 4 tukiwa kampuni moja tulifanikiwa kupata mtoto na mwenzi wa 12, mwanetu anatimiza miaka 4 Mungu akipenda. Kumekua na tatizo ambalo sasa limekua sugu kwani sio mara ya kwanza wala yapili kutokea
Kama tunavyo fahamu matatizo kwenye mapenzi yapo tu hilo halipingiki ila kutafuta solution hilo ndio swala la msingi lakin Mimi kila tukikwaruzana na mwenzangu kosa liwe langu au lake yeye kikubwa anachotangulizaga ni kuondoka na kukomba vitu vya ndani
Kitendo hicho alishanifanyia zaidi ya mara moja lakini kila ikipita muda wiki tatuu hadi mwezi hua anarudi na machozi kujifanya anajutia hua anatumia mlango wa wazazi wangu kuomba msamaha mwisho wa siku kwakuwa nampenda hua namsamehe na kusonga mbele na kuachana na yaliyo pita.
Hivi majuzi tuligombana pia chanzo kikubwa ni simu kwani kila anaporudi nyumbani mwenzangu yuko busy na simu kujifanya Ana report zakutuma nk.
Lakin tabia hiyo siku hadi siku ikazidi kukomaa kwani imefika hatua mpaka muda wa kulala yuko busy hata nikimsogelea hataki ikabidi nikae kimya nifanye utafiti nijue shida ni nini au mchawi ni nani nilichofanya nikachukulia u-busy wake kama kitu cha kawaida na usumbufu wa usiku nikaacha kwani kila usiku nimekua wakulala na masononeko mwenzangu akiwa busy na simu
Mwisho wa siku nawaza mpakaa napitiwa na usingizi nikishtuka gafla nakuta bado anaendelea hivo hivo nikiuliza ndo nakua nimezua ugomvi na kununiwa wiki nzima.
Nielendelea kuwa mvumilivu nikiwa na target yangu yakutaka kujua kinacho endelea kwenye hiyo simu yake kwani simu yake App zake Ali lock kwa finger print ikafika siku ya siku sasa nilitangulia mimi kulala kama kawaida nayeye akiwa amejilaza huku Ana chart simu yake
Kila nikimuombaga huwa nakuta chat zimefutwa kama ilivyo za mwizi ni 40 siku hiyo nilipo lala na yeye akachart na usingizi ukampitia alipoanza kukoroma nikaichukua simu yake nikatoa lock kwa kidole chake ndipo mchele ulipo mwagika kumbe mwenzangu alikua na mahusiano mapya na jamaa mwingine
Wakati naendelea kupekua pekua akashtuka sikusita kumuuliza kwani nihakiyangu kuuliza cha ajabu mwanamke alicho nijibu ni kwamba yeye ni mrembo tena yeye ni namba D anatongozwa kila siku na kunambia maisha anayaweza sio lazima kua na mimi. Iliniuma kwanamna nlivyokua nimejitolea kwake nikajikuta hatakuongea tena siwezi kwani walikua wamepanga na appointment tena ya kukutana njeee ya mji nilishikwa na hasira kiasi cha kumpatia kichapo nilipo taka kuchukua simu nibaki na evidence akaipasua ikatawanyika kila kitu palivyo kucha akaenda police kunikatia RB
Kwani maelezo aliyoenda kutoa nikwamba Mimi namtesa nampiga kila siku na hiyo simu nimevunja Mimi anataka nilipe nilikaa sero kwa muda lakini nikapewa nafasi ya kutoa maelezo yangu walipo sikiliza na kupima huku na huku wakasema tukae dawati mwanamke akakataa na kusema kama imeshindikana sheria kufata mkondo wake yeye anataka Mimi na yeye tuachane
Kikubwa alitaka niende jela nikakubaliana na yeye tukaenda nyumbani akachukua vitu vyake na kuondoka na kuniachia mtoto hapo nilishukuru kwani nilikua na hofu sana juu ya kumkosa mwanangu alipo ondoka kwao hakuenda akaenda kwa shoga yake kuishi imepita miezi 5 sasa alikuja mara moja tu kumuona mtoto kuhusu hilo i don't care.
Sasa amekua ni mtu wakunichafulia jina kila mahali kila mahali anapopita nikuongea mambo yasiyo faa na yasio na ukweli ndanii yake baadhi ya staff wenzangu pia kunitenga kupitia maneno yakee
Hapo hapo pia boss anamtaka mke wangu sasa boss ananiandama na kunitafutia sababu kila siku japo kua majukumu yangu natimiza inavyo takiwa nashindwa hata nifanye nini kila nnapopita nimekua wakunyooshewa vidole lakini nikasema hakuna haja ya kumuelezea yoyote matatizo yangu kwani naona kama nikujichoresha na kufaidisha watu lakini kinachoniumiza pia jamii inayo nizunguka watu nnao shirikiana nao kikazi sasa wako against me kutokana na maneno aliyo spread mwanamke huyo matokeo ya kumpoteza nimekubaliana nayo lakin maneno yake juu yangu sasa imekua too much na mimi sitamani wala sihitaji kusogea karibu yake wala kuzungumza nae kwani jeraha la moyo wangu laweza nisukuma nikafanya kitu ambacho Sio dhamira yangu nifanye nini wakuu?
By Rahul Pacquao
Tags