Paul Makonda "Migogoro mingi Dar tumeitatua"
0
June 26, 2020
Mwaka 2016 RC Paul Makonda akiwa kwenye ziara DSM ya kukagua utekelezaji wa shughuli za Serikali na kusikiliza kero za Wananchi aligundua wengi walikua na uelewa mdogo wa Sheria ambao uliwapelekea kupoteza haki zao za msingi, kutapeliwa, kudhulumiwa ama kutojua mahali sahihi pa kupelekea malalamiko yao.
Baada ya ziara, RC Makonda aliwatafuta Wanasheria 35 waliokua tayari kujitolea kwa kutoa msaada wa kisheria bure kwa wananchi wa DSM na Dec 16, 2016 aliwakabidhi kwa Ma-DC wa DSM ili wawe msaada katika ofisi zao pale wananchi wanapofika kuelezea matatizo yao yanayohitaji suluhisho la kisheria.
Kiongozi wa Wanasheria hao 35 amesema, jumla ya malalamiko yaliyopokelewa kuanzia Dec 26,2016 ilipoanza kazi hadi sasa ni 1,758,204 pamoja na wananchi 3,098,773 ( kuna migogoro yenye walalamikaji zaidi ya 100,000).
Migogoro 1,354,092 imeweza kutatuliwa pamoja na wananchi 2,034, 932 wameweza kutatuliwa matatizo yao ya kisheria.
Tags