Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema fomu ya urais zitaanza kutolewa kuanzia Juni 15 hadi 30, 2020.
Amesema nafasi ya ubunge ndani ya chama fomu zinachukuliwa kuanzia Julai 14 na mwisho wa kurejesha Julai 17, 2020.
''Ratiba ya kumpata mgombea nafasi ya Rais wa Tanzania inaanza Juni 15 - 30, 2020 ambapo itakuwa nafasi ya kuchukua fomu, kutafuta wadhamini na kurejesha fomu . Muda ni Saa 10:00 jioni'' - @hpolepole#CCMPress pic.twitter.com/kNgr2XuRtb— eastafricatv (@eastafricatv) June 12, 2020