Polisi Aliyemuua Mmarekani Mweusi Kwa Kumpiga Risasi Mbili Mgogoni Aingia Matatani...
0
June 15, 2020
Afisa wa polisi aliyemuua Mmarekani mweusi katika mji wa Atlanta huko Marekani, anaweza kushtakiwa katikati ya wiki hii, kulingana na mwendesha mashitaka mkuu wa kaunti ya Fulton, Paul Howard.
Howard amesema ofisi yake itazungumza na mashahidi wengine wawili, kabla ya kufanya uamuzi wa kufungua mashtaka dhidi ya afisa, Garrett Rolfe. Kulingana na uchunguzi wa jimbo la Georgia, afisa huyo wa polisi alimpiga risasi Rayshard Brooks mwenye umri wa miaka 27 akiwa nje ya mgahawa mjini Atlanta Ijumaa usiku, baada ya kijana huyo kukataa kukamatwa.
Howard alikieleza kituo cha televisheni cha Marekani, CNN, kwamba Brooks hakuonekana kama ni tishio kwa mtu yeyote, kwa hiyo hakujakuwa na haja ya kumuua. Brooks alifariki kwa kupozeta damu nyingi, baada ya kupigwa risasi mbili mgongoni.
Na kifo chake kimeorodhoshwa kuwa ni mauaji.
Tags