Polisi Sita Kushtakiwa kwa mauaji Wakati wa Marufuku ya Kutembea Usiku Kenya




Polisi 6 watashtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyanyasaji, kwa kuhusishwa katika matukio ya kufyatua risasi dhidi ya raia wakati wakihakikisha marufuku ya kutotembea usiku inatekelezwa

Ripoti ya mamlaka inayoangazia makosa ya Polisi nchini humo (IPOA) imesema, Wakenya 15 wameuawa na Polisi katika kipindi cha marufuku ya kutotembea usiku ili kudhibiti maambukizi ya CoronaVirus

Ripoti nyingine ya #HakiZaBinadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema kuwa kulikuwa na ghasia za Polisi katika jamii zipatazo 182, vurugu hizo zilijumuisha kupiga watu, kurusha mabomu ya machozi, unyanyasaji wa kingono na kuharibu mali za watu

Kati ya watu waliouawa ni Yassin Moyo(13) aliyeuawa Machi 28. Yassin amedaiwa kupigwa risasi tumboni na Polisi siku moja baada ya marufuku ya kutembea usiku kuanza kutekelezwa
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Poleni wafiwa na kenya kwa Ujumla wake.

    CORONA haitembezwi kama pipi..!!

    Busara / Hekima na UTU. ni vyema vitumike na Kila mwenye Jukumu lake katika mpito huu wa Lokidawni ya kujitakia.

    Sisi Watanzania hatuna vyote. Si lockdown wala wa-athirika kama ilivyo tabiriwa.

    Msiue watu. It does not deserve.

    ReplyDelete

  2. https://youtu.be/AA8WGpFTafI




    CORONA haitembezwi kama pipi..!!

    Busara / Hekima na UTU. ni vyema vitumike na Kila mwenye Jukumu lake katika mpito huu wa Lokidawni ya kujitakia.

    Sisi Watanzania hatuna vyote. Si lockdown wala wa-athirika kama ilivyo tabiriwa.

    Msiue watu. It does not deserve.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad