Polisi washambuliwa na waandamanaji nchini Uingereza




Polisi walishambuliwa kwa chupa wakati wa makabiliano kati yao na mamia ya waandamanaji mjini London, ambao walipuuza agizo la kutoshiriki maandamano.


Makundi ya watu yalikusanyika katikati ya mji mkuu,wakidai kuwa wanalinda sanamu dhidiya wanaharakati wanaopinga ubaguzi wa rangi.

Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yamefanyika katika miji tofauti nchini humu ikiwa ni pamoja na mii wa London.

Polisi wameweka masharti dhidi ya makundi kadhaa, kufuatia vurugu mbaya zilizoshuhudiwa wikendi iliyopita.

Makundi kadhaa kutoka sehemu tofauti nchini, pamoja na wanaharakati wa mrengo wa kulia, yalisema yamekuja mjini London kulinda alama ya historia ya Uingereza.

Mamia ya watu wengi wao wazungu walikusanyika katika ukumbi wa ukumbusho wa Cenotaph katika eneo la Whitehall amble linapakana na sanamu ya Winston Churchill iliyopo karibu bunge.

Makabiliano yameripotiwa kati ya polisi na waandamanaji ambao walikuwa wakisema kwa pamoja “England” huku wakiinua mikono yao kuelekea walipo maafisa wa polisi.

Baadhi yao walifanikiwa kuvunja uzio wa chuma unaozunguka Cenotaph katika eneo la Whitehall na kuanza kuwarushia polisi milingoti ya umeme na vifaa vingine walipokuwa wakijaribu kuwadhibiti.

Waadamanaji hao baadae walielekea Trafalgar Square, ambapo walianza kurusha fataki kuelekeakwa makundi ya yatu.

Polisi walikuwa na kibarua kigumu kuwazuia wasifike katika bustani ya Hyde Park ambako kulikuwa na mandamano ya amani ya watu wanaopinga ubaguzi wa rangi.

Wasimamizi wa vugu vugu la Black Lives Matter walikuwa wametoa kwa watu kutoshiri maandamano ya kupinga ubaguzi yaliyopangwa wikendi hii kwa kuhofia huenda yangegongana na makundi ya marengo wa kulia.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad