Rais Magufuli amempigia simu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na kutoa maagizo “Suma JKT waache kuwapigisha ‘kichura chura’, hapo (Dodoma Stand) sio jeshini,hao mmeingia nao mkataba wa kulinda usalama wa raia, hawapo hapo ili kuwapigisha Watu vichurachura na bahati nzuri Suma JKT wanafanya kazi nzuri hawajaanzia stendi ya Dodoma”.
“Suma JKT wanafanya kazi nzuri hawajaanzia stendi ya Dodoma, wapo pale Feri DSM, Mwanza hatujaona Watu wakipigishwa vichurachura, wanaofanya hivyo waondolewe mara moja, wabaki maaskari wanaowahudumia watu, sitaki watu wangu warushwe vichura kwenye nchi ya amani”-JPM