Rais Magufuli aitaka Wizara ya Afya kuongeza bajeti katika dawa za asili




Rais John Pombe Magufuli ameitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuweka nguvu na kuongeza  bajeti katika Kitengo cha Tiba asili/tiba mbadala ili kutengeneza dawa za asili kwa ajili ya kuponya magonjwa mbalimbali.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akizindua Jengo la Ofisi za TARURA zilizojengwa kwenye mji wa Mtumba.

"Nimeshatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya, kile kitengo cha dawa asili kiendelezwe kwa nguvu zote na bajeti iongezwe ili watu wanapotengeneza dawa zao tusiwadharau," amesema Rais Magufuli.

Amesema dawa za asili zinasaidia kutibu magonjwa mbalimbali  na kwamba zimesaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini.

Rais amewataka Watanzania wabadilike na wapende dawa za asili zinazotengenezwa nchini kwani wamekuwa wakipumbazwa wasiziamini, hivyo amewataka waziamini na kuzitumia kwa kuwa zinaponya. 

“Dawa za asili zinasaidia kujifukiza, zimesaidia sana, Corona haijaisha ila imepungua sana.Waliotegemea tutakufa wengi na barabarani patakuwa na maiti, wameshindwa na walegee kweli kweli,” amesema Rais Magufuli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad