RAIS Dk.John Magufuli amesema huwa anasikitishwa kuona watu ambao wamewapa nafasi na kuwaamini wanashindwa kutekeleza yale ambayo amewatuma kwenda kufanya na badala yake wanakwenda kufanya ya kwao huku akitumia nafasi hiyo kuzungumzia vijana ambao amewapa nafasi lakini hawaridhiki nazo.
Akizungumza leo Juni 22, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta , Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele ,Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa,Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima pamoja na Mkurugenzi wa Kaulia Jerry Pima.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozio waliokuwa kwenye nafasi kutekeleza majukumu yao kwa kushemu sheria na viapo walivyoapa kikiwemo kiapo cha maadili ya viongozi wa umma.
“Niliwaapisha leo nendeni mkazingatie viapo vyenu, mmeampa viapo vya maadili nendeni mkazingatie.Huwa nasikitika ninapoona watu ambao umewateua na kuwaapisha lakini wakienda maeneo yao ya kazi hawafanyi kazi viapo vyao.
“Mkoa wa Arusha katika kipindi cha miaka miwili Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji Arusha walikuwa hawalewani ,wao ni kugombana tu.Walikuwa wanafanya kazi lakini waliniudhi kwa kutoshirikiana.Sasa nimeateua ninyi sitaki yakatokee hayo.Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kafanyeni kazi zenu vizuri, “amesema .
Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa tatizo la vijana ukiwapa nafasi wanashindwa kuridhika na hizo nafasi, wanasahau miaka bado ni mingi sana. “Kwasababu TAKUKURU na IGP mpo hapa nendeni mkawaonye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha pamoja na Mkuu wa TAKUKURU Arusha.
“Ilikuwa niwatoea ila nimewasamehe, lakini sijawasamehe moja kwa moja wakifanya makosa nawaondoa. Wafanye kazi ambazo nimewatuma na badala ya kwenda kufanya kazi zao.Mnafahamu kazi ambazo walikuwa wanazifanya katika kipindi hiki kifupu, nendeni mkaawambie wafanye kazi nilizowatuma, wasimame maadili, wasimamie sheria,”amesema Rais Magufuli.
Wakati huo huo Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenda kutatua migogoro ya ardhi iliyopo katika baadhi ya wilaya katika mkoa huo.Kulikuwa kuna mgogoro wa Kanisa na Shule, kulikuwa na maamuzi kwamba litafutwe eneo lingine na Jiji lilipe Sh.milioni 400 .”Nilishatoa maamuzi wakitaka kuongeza shule wajenge ghorofa lakini sio kwenda kutafuta eneo jingine.”
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuna eneo la wazi ambalo kwa muda mrefu viongozi wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakiiomba eneo hilo lakini msimamo wa viongozi wote waliopita kuanzia awamu ya pili mpaka awamu ya nne wametoa maelekezo eneo hilo kubaki kama lilivyo laini na sasa limeibuka tena.
“Openi space inabaki kuwa open space, mgogoro ulianza enzi ya Mze Mwinyi akakataa, mzee Mkapa akakataa, mzee Jakaya Kikwete kakataa, na sasa limeletwa tena kwangu.Msimamo ni ule ule ambao uliwekwa na viongozi waliotangulia.
“Ila ikitokea shughuli kwa mfano Maulid au ibada nyingine yoyote ya kidini eneo hilo litumike bure.Tatizo limeletwa na Mkuu wa Mkoa ili aonekane mzuri.Hivyo wewe Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi msiingie kwenye tatizo hilo,”amesema Rais Magufuli.
Amezungumzia pia ujenzi wa stendi ya mabasi ya Mkoa wa Arusha ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kuhakikisha anakwenda kufanikisha ujenzi huo.
“Mkasimamie hilo wanannchi wa Arusha wamecheleweshwa kupata stendi.Viongozi waliopita wamekuwa wakibishana sasa wakabishanie huko mtaani.Kama kugombana na kubishana kabishane na mkeo na mtoto wako.Ni matumani yangu ninyi ambao nimewateua mtakwenda kufanya yale ambayo tunayatarajia.Arusha tumepeleka miradi mingi mno na wana arusha wanafahamu,”amesema Rais Magufuli.