Rais Magufuli awataka DC na DED wa jiji la Dodoma waoe




“Dodoma ndio kila kitu, kwahiyo wewe Mkurugenzi (Kunambi), ni Mkurugenzi wa Jiji la Makao Makuu hata kama ni mdogo, ila utafute Mwanamke uoe, kwani hawapo Wanawake wanaotaka kuolewa na Mkugenzi jamani!?, nimekutangazia uanze kutafuta ndoa, DED unajipikia wakati Wagogo wapo wengi”-JPM 

“Mkuu wa Wilaya Dodoma (Katambi) pia nae hajaoa kama DED (Kunambi), lazima tusemane hapahapa, na wewe uoe, huwezi kukaa na Viongozi wakubwa wa Makao Makuu hawana Wake, wakati Wasichana wapo wanapita hapa wengine wapo UDOM, CBE, Mipango wewe huoni tu!?”-JPM 

“DC Dodoma na DED Dodoma mnataka muambiweje (ndio muoe), maana nyinyi sio Mapadri, sasa macho yenu hayaoni!?, wewe Nchimbi una Mke eeh? haya waambie hawa waoe..nilikuwa nachomekea tu kwamba tupo kwenye Makao Makuu ila tunaongozwa na Vijana ambao hawajaoa”-JPM

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Karibuni nyumbani tuzungumze mikakati ya
    Ndoa na uchagui wa mama mtarajiwa anae weza kuwa mama familia yenye maadili

    https://youtu.be/AA8WGpFTafI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadakta mdau, tuwaozeshe wake wema!

      Delete
  2. Ushauri n wazo ni Zuri sana. Toka kwa Mzazi kwa wanae.

    Tuko tayari kuwapeni Wake. Karibuni Mlowa Barabarani , Nondwa kwetu n hata Mkonze na Tubugwe juu. Tuna mabinti na Mahari siyo kubwa tunayoitaka. Ni NDAMA
    jike Mbili tu inatosha.

    Njooni tuwape wake.

    Najalibu kutoa location ya goggle ili mfike wanangu!

    https://youtu.be/AA8WGpFTafI

    ReplyDelete
  3. Leo asubuhi tulikuja kunya Kahawa kwa Mzee Ndahani, katika mazungumzo kufuatia ushauri wa mh JPJM. Mzee Ndalu kasema yuko tiyari kuwaozesha binti zake wawili
    (Scolastika na Magidalena) mahari mbuzi 4 na kondoo 6.

    Sasa mimi na Mzee Chidegwa, Tuko tiyari
    kusaidia. Jipangeni Vijana mkiwa tiyari mtujulishe. ili tuweze Kulimaliza hili Jambo ki uchamungu. Hongereni wanangu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad