Rekodi kubwa 5, ubingwa wa 19 wa Liverpool
0
June 26, 2020
Klabu ya soka ya Liverpool imefanikiwa kushinda ubingwa wa ligi nchini Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 na kufikisha ubingwa wa 19 nyuma ya mahasimu wao Man United wenye mataji 20.
Ni baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Chelsea na Manchester City, ambao ndiyo walikuwa kizuizi kwa Liverpool katika kushinda ubingwa kutokana na kuwepo kwa uwezekano wa kuzifikia pointi zake kabla ya mchezo huo wa jana.
Mabao 2-1 waliyoshinda Chelsea kupitia kwa Willian na Christian Pulisic yalitosha kupelekea furaha Anfield na kuzalisha rekodi mbalimbali.
Rekodi ya pili: Liverpool imeshinda ubingwa zikiwa zimebakia mechi 7 ligi kuisha, ikiwa ni klabu ya kwanza kufanya hivyo ikiizidi rekodi iliyowekwa na klabu za Man United (1907/08 na 2000/01), Everton (1984/85) na Man City (2017/18).
Rekodi ya tatu: Msimu wa 2019/20 umekuwa msimu wa tatu kati ya sita ya hivi karibuni ambayo mechi ya kuamua ubingwa imechezwa katika uwanja wa Stamford Bridge, mechi zingine ni Chelsea Vs Crystal Palace 2014/15 na Chelsea Vs Tottenham 2015/16.
Rekodi ya nne: Ubingwa wa Liverpool umekuwa na mkusanyiko wa rekodi kadhaa ambazo wamezipata ndani ya msimu huu, ikiwemo kushinda mechi 18 mfululizo, kushinda mechi 23 mfululizo za nyumbani, kushinda ubingwa wa ligi kwenye miongo 8 tofauti na kutokufungwa katika mechi 44 za mashindano yote.
Rekodi ya tano: Msimu huu Liverpool imeifunga kila klabu iliyokutana nayo katika ligi angalau mara moja, ikiwa ni historia ambayo haijawahi kuwekwa na klabu hiyo hapo kabla.
Tags