Sababu za Korea Kaskazini kulipua ofisi za mawasiliano na Korea Kusini zaelezwa



Korea Kaskzini imeafikia vitisho vyake vya kulipua afisi ya uhusiano wake na korea kusini hatua ilioshituwa ulimwengu mzima. Kuanzishwa kwa ofisi hiyo ilikuwa ni sehemu ya misururu ya hatua za maridhiano ambazo zilifanywa mwaka 2018 baada ya viongozi wa mataifa hayo ya Korea ambao kiuhalisia bado wapo katika vita, kuboresha uhusiano wao.



Baada ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un kukutana mwaka 2019, kulikuwa na matumaini kuwa Korea Kaskazini itaachana na mpango wake wa silaha za nuklia .

Lakini hamna ambacho kimefanyika tangu mkutano huo ufanyike.

Katika miezi ya hivi karibuni , kumekuwa na uvumi kuhusu uhalisia wa hali ya virusi vya corona Korea Kaskazini -ambayo ilidai kuwa haina maambukizi ya virusi hivyo vya corona na hali ya uchumi kudaiwa kushuka.

Kulikuwa na uvumi pia kuhusu hali ya kiafya ya kiongozi wa taifa hilo bwana Kim Jong-un kuwa anaumwa na hivyo dada yake anaandaliwa kuchukua nafasi yake kama kutakuwa na uhitaji huo.

Lakini kwa nini Korea Kaskazini imeamua kuchukua hatua hiyo na ina maana gani?
Wachambuzi kutoka taifa hilo wanaeleza;

line break
‘Pyongyang inaweza kusababisha janga’ – Ankit Panda, ni mwandishi wa Kim Jong Un na alinusurika bomu: Kunusurika na kusalia Korea Kaskazini

Muda mfupi baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 na mwaka mmoja wa mkutano wa pamoja wa Korea, ofisi ya mawasiliano ya mataifa hayo mawili imeharibiwa na tukio hilo kukumbusha namna ambavyo uhusiano huo ulivyoenda vibaya tangu miaka ya nyuma na jinsi jitihada za sasa zinavyovurugika haraka mno.

Upande wa Korea Kaskazini, ulitoa taarifa ya wazi kuhusu hatua hiyo na kutaja shughuli ambazo makundi ya wanaharakati wa Korea Kusini yamekuwa yakifanya na hivyo kusababisha Korea kaskazini kufikia maamuzi hayo.

Siku zijazo tunaweza kuona Korea Kaskazini ikichukua hatua nyingine zaidi kama wanajeshi kufanya mazoezi, kupiga risasi katika ukingo wa Korea Kusini au kufanya matukio ambayo walikuwa wanataka kuyafanya kabla ya makubaliano ya mataifa hayo ya Septemba, 2018.

Lakini kuhusu lengo na mkakati wa uchochezi huo hakuna kilichowekwa wazi.

Pyongyang inawezekana inatafuta namna ya kuanzisha mgogoro ili kumhamasisha rais wa ,Korea Kusini Moon Jae-in, ambaye ana viti vingi bungeni kuendeleza miradi ya ushirikiano kiuchumi wa mataifa hayo.

Ukiachana na uchochezi huu na mingine ambayo inatarajiwa , inaweza kuhusishwa na juhudi za ndani za kujenga nguvu za dada yake Kim Yo-jong, Kim Jong-un. Hata hivyo yeye ndiye aliyetangaza kuharibiwa kwa ofisi ya mawasialiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

line break
Dada yake ‘Kim Jong-un yuko mbele na kati’ – Andray Abrahamian, Profesa wa chuo kikuu cha George MasonKorea
Je Kim Yo Jong anatayarishwa kuongoza Korea kaskaziniJe Kim Yo Jong anatayarishwa kuongoza Korea kaskazini
Kumekuwa na uvumi wiki chache zilizopita kuwa Korea Kaskazini inataka kuondoa baadhi ya posho Korea Kusini , na inataka Marekani kufahamu kile ambacho wana uwezo wa kukifanya bi;a kujaribu makombora yao ya masafa marefu au wanataka kuanzisha vurugu ili yavutia mazungumzo ya dharura .

Hakuna mkakati hata mmoja ambao unaridhisha kwa ujumla .

Wakorea wa Kaskazini wengi hawana mbadala wa siasa za ndani na hawana uhakika wa kile ambacho kinaendelea.

Ukweli kuhusu dada yake mdogo Kim Jong-un kuwa upande wa kati na mbele umeweza kuleta taharuki ya kumjenga kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi kwa wapinzani wa Korea Kaskazini.

Pamoja na kwamba alihusika katika makubaliano ya uhusiano wa mataifa hayo ya Korea mwaka 2018.

Sasa viongozi wanataka kuuonyesha umma kuwa sio mtu wa kumchezea na mataifa ya kigeni kupata ujumbe kuwa kama Pyongyang imeachana na rais wa Korea kusini Moon Jae-katika kuvunja uhusiano wake na Marekai ili kuangazia ushirikianao wa Korea , basi ni muhimu kufikiria kwamba hawana cha kupoteza.

line break
‘Korea Kaskazini inahisi imesalitiwa na Trump’ – Van Jackson, mwandishi wa kitabu cha ‘ Brink’: Trump, Kim, na vitisho vya vita ya Nuklia
North Korean leader Kim Jong Un and U.S. President Donald Trump inside the demilitarized zone (DMZ) separating the South and North Korea on June 30, 2019 in Panmunjom, South Korea
Motisha huo wa shambulio unaonesha kuhusishwa na masuala matatu.

Moja ni kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anahisi kusalitiwa baada ya makubaliano ya mkutano na rais wa Marekani Donald Trump kutotekelezwa .

Kim aliingia kwenye hiyo mikutano akiwa na matarajio ya kukuza uchumi wake lakini ameambulia patupu.

Pili, Uchumi wa Korea Kaskazini umeshuka kufuatia janga la corona baada ya kushindwa kufanya biashara na China mbali na kampeni za Marekani za kuiwekea vikwazo.

Tatu, dada yake Kim Jong-un yuko kwenye jitihada za kujijengea jina na anapaswa kuonyesha makali yake kwa wananchi wote na wanajeshi wa zamani wa Korea Kaskazini.

Ingawa haijawekwa wazi kama dada huyo ndio atamrithi kaka yake ambaye anadaiwa kuumwa.

Sababu ya kuilenga Korea Kusini ni mkakati kwasababu Korea Kaskazini inahatarisha mgogoro wa muda mrefu iwapo itaishambulia Marekani moja kwa moja hivyobasi inalenga Korea Kusini ili kuzuia kusababisha vita.

 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad