Sakata la ofisi ACT Wazalendo yawataka CUF kwenda mahakamani sio kwenye vyombo vya habari



Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema kama CUF wanadai Ofisi zao zilizopo Zanzibar zimechukuliwa, basi wapeleke malalamiko yao Mahakamani na siyo kwenye vyombo vya habari

Amesema Chama hicho kuanzia Juni 22, 2020, kitafungua rasmi mlango kwa watia nia wa kugombea nafasi za Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na kimejipanga vilivyo na hakiendi kwa kufuata mkumbo bali wanaenda kwa kuwa wamefanya maandalizi muhimu

Amefafanua, "Mtu anasema ana ofisi mwambie aoneshe hati ya kiwanja, CUF hawana jengo wala gari hata moja. Hizo ni mali za watu binafsi ambao walikiazima chama cha CUF wamekichoka, wamechukua mali zao. Ingelikuwa mtu kachukua mali ya mtu, wangekamatwa na kuwekwa ndani kwa uvamizi, iweje sisi ambao tumechukua mali tuwe tunadunda barabarani na wengine wanazidai kwa Press conference, mali zinadaiwa Mahakamani waende"

Aidha, Katibu Mkuu huyo ameongeza, "ACT ni chama ambacho kinaenda kuonesha kwamba ni mbadala wa uhakika kinachobeba maono na matumaini ya Watanzania na kesho sisi tutatoa mwelekeo mpya wa chama chetu tutaonesha sehemu ya nguvu zetu, Zitto na Maalim watazungumza na huo ndiyo utakuwa mshindo wa kwanza"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad