Serikali ya China imepanga kuanza utaratibu wa kuwapa wananchi wake vocha za kufanyia manunuzi mtandaoni, madukani, mahoteli, utalii na michezo kama njia ya kuongeza kasi ya ukuaji uchumi. Tayari dola bilioni 1.7 zimetengwa kwa ajili hiyo.
Manunuzi katika biashara za rejareja yamepungua kwa 20.4% tangu mwaka uanze kufuatia ugonjwa wa Covid-19.