Serikali ya Congo Yatangaza Kumalizika kwa Ugonjwa wa Ebora



Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetangaza rasmi kumalizika kwa janga la ugonjwa wa Ebola ambao ulizuka katika eneo la mashariki mwa Nchi hiyo Agosti mwaka 2018 na kusababisha vifo vya watu 2,277.

Waziri wa afya wa Nchi hiyo Eteni Longondo amesema kuwa kuzuka kwa ugonjwa huo, kulidumu kwa mrefu zaidi, pamoja na ugumu wa matibabu na wa hatari, katika historia ya miaka 60 ya nchi hiyo.

Eneo la mashariki mwa Nchi hiyo limeadhimisha rasmi kumalizika kwa ugonjwa huo uliodumu kwa karibu miaka miwili wakati makundi yenye silaha na jamii kutokuwa na imani kulivuruga ahadi za kuwa na chanjo mpya.

Zipo changamoto nyingi za kiafya ambazo bado Congo inakabiliana nazo, kubwa zaidi ikiwa ni janga la ugonjwa wa surua, ongezeko la kitisho cha ugonjwa wa COVID-19 pamoja na kuzuka upya kwa ugonjwa wa Ebola upande wa Kaskazini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad