Mahakama moja nchini Afrika kusini imetangaza kuwa sheria zinazohusika katika kuwazuwia watu kutotoka nje ni batili kufuatia kupingwa kisheria na taasisi ya kiraia kwa misingi kwamba inakwenda kinyume na katiba.
Mahakama kuu ya jimbo la Guateng imeipa serikali siku 14 kubadilisha sheria hizo katika njia ambayo haiendi kinyume na haki za raia. Hatua ya Afrika kusini kuwazuwia watu kutzoka majumbani mwao ilinza Machi 27 na imekuwa ikilegezwa taratibu.
Lakini bado inapiga marufuku kuuzwa kwa sigara na kuzuwia biashara nyingi na viwanda kufanyakazi kwa kiwango chake cha juu.
Utaratibu huo wa serikali pia uhazuwia mikusanyiko ya watu na kuzuwia watu kuhudhuria katika mazishi kwa zaidi ya watu 50 .
Serikali imekubali uamuzi wa mahakama hiyo na kusema itachukua hatua mara itakapoichunguza hukumu hiyo.