Serikali Yataifisha Dhahabu ya zaidi ya Tsh. Billion 2.9



Serikali imetaifisha dhahabu ya Kilogram 27.488 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9 iliyoingizwa kinyemela kutoka Kenya
-
Dhahabu hiyo mali ya Mfanyabiashara Bhawesh Chandulal Gandecha, ilikamatwa na Afisa Forodha katika mpaka wa Tanzania na Kenya huko Sirari, Mei 15, 2020
-
Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Wallace Mkande, amesema Mfanyabiashara huyo alikamatwa akitaka kuingiza dhahabu hiyo kutoka Kenya kinyemela bila kuwa na nyaraka za kuonesha amelipia ushuru
-
Mfanyabiashara huyo alipoulizwa alisema ameshalipa ushuru ila hajapewa stakabadhi na kuwa nyaraka nyingine zipo Dodoma huku akipiga simu kwa baadhi ya watu kuwalalamika kwa kushelewesha kuzituma
-
Alifunguliwa kesi Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kushtakiwa kwa makosa ya Kuendesha Mtandao wa Uhalifu, Kufanya biashara ya dhahabu bila nyaraka muhimu na kutakatisha fedha

#JamiiForums - #regrann

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad