Siku za Mwizi ni Arobaini...Wezi wageuzwa Kuwa Kama Ng'ombe Huko Butiama


Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wezi wa mifugo katika Kijiji cha Busegwe Wilayani Butiama Mkoani Mara, wamekumbwa na hali ya kula majani kama Ng'ombe, mara baada ya wanakijiji kushirikiana na familia iliyoibiwa Ng’ombe, kumuita mganga kutoka nchini Kenya na kufanya dawa hiyo.

Imeelezwa kuwa tukio hilo la aina yake limetokea jioni ya Juni 15, 2020, ambapo lengo kuu la kumuita mganga huyo, ilikuwa ni kuwarudisha watu waliomuiba Ng'ombe mwenye thamani ya Shilingi Milioni 2 kwa kuwa tabia ya wizi wa mifugo kijijini hapo, imekithiri kwa kiasi kikubwa.

Imeelezwa kuwa mara baada ya dawa hiyo kufanyika, watu hao walirudi na kuanza kukata majani na kuyala kama wafanyavyo Ng'ombe, kitendo ambacho wamekifanya wakiwa kwenye hali ya kutojitambua, huku wakishuhuduwa na wana Kijiji.

Kwa upande wake mmiliki wa Ng'ombe aliyeibiwa Grace Jonathan, ameeleza ni kwa namna gani alibaini kama mfugo wake hayupo zizini, "Ng'ombe huyo aliibiwa usiku wa kuamkia ijumaa(Wiki iliyopita), mwanzo hatukugundua lakini, watoto wakati wanaenda kuchunga ndiyo tukabaini kwamba Ng'ombe hayupo, tukaja kuangalia Zizi la Ng'ombe limekatwa, moja kwa moja tukajua kaibiwa kwahiyo msaada mbadala ndiyo tulioutumia, na ndiyo hiki mnachokiona hapa". 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad