Sugu: Kutoka Ndoto ya Kuwa Padri hadi Muziki na Baade Ubunge


Katika kitabu chake cha SUGU THE AUTOBIOGRAPHY -MAISHA NA MZIKI (FROM THE STREET TO THE PARLIAMENT) Sugu anasema

""Nakumbuka katika kipindi hicho nilikuwa karibu sana na kanisa, nilikuwa mmoja wa wahudumu waandamizi wa kanisa kuu la Watakatifu wotela mjini Mtwara, kanisa ambalo ndipo nilipobatizwa… nilitumia muda mwingi wa ziada baada na pengine hata kabla ya kwenda shule kuwapo katika kanisa hili, kila siku ilikuwa ni lazima niende nikahudumie katika misa ya saa kumi na mbili asubuhi kwanza ndipo niende shuleni

Nililipenda sana kanisa na pia Imani yangu yangu ya ukatoliki, kiasi nikawa na ndoto kwamba siku moja niwe sio tu Padri bali bali Askofu kabisa! Nakumbuka nilivutiwa sana na Paroko wa kanisa hilo ambalo Mtwara linajulikana kwa ufupi kama kanisa la Parish, Father Gallus Chilamula, Pia nilivutiwa na askofu wa jimbo la Mtwara wakati huo marehemu marehemu baba askofu Maurus Libaba

Ndoto ya kuwa Padri zilianza kutoweka na hatimaye kupotea kabisa baada ya kuhamishwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam kwa mama na baba yangu kusoma hiyo ikuwa mwaka 1984 mwishoni nikiwa darasa la nne kuingia la Tano."""

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Kumtambulisha Mch Msigwa!!

    https://youtu.be/EpBDiKuNabY

    Kula yetu tunakupa!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad