Timu ya Simba Wanautaka Ubingwa Wao



SIMBA wanautaka ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara baada ya nahodha na mshambuliaji wa timu hiyo, John Bocco, kusema sasa wapo tayari kuendelea na mechi zilizobaki kumalizia kazi ya kubeba ubingwa.

Bocco ametoa kauli hiyo Simba ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 71 baada ya kucheza mechi 28. Imebakiwa na mechi kumi kumaliza msimu huu ambapo kati ya hizo, ikishinda tano tu inakuwa bingwa.

Akizungumza na Spoti Xtra, Bocco alisema: “Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mapambano ya kumalizia ligi, tunachosubiria ni kuingia uwanjani na kuanza kupigania ubingwa wetu katika sehemu ambayo imebaki.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad