Trilioni 13 zatolewa Kumaliza mji wa Msanii Akon Unaitwa Akon City



Staa wa muziki Afrika na Marekani Akon, amepokea kiasi cha Tsh Trilioni 13 kutoka kwa kampuni ya uhandisi nchini Marekani kwa ajili ya ujenzi wa mji wa Akon City nchini kwao Senegal.

Akon aliingia mkataba wa ujenzi huo mnamo Juni 6, 2020 na alipokea pesa hizo kutoka kwa wawekezaji ambao wanataka kukuza maendeleo ya mji huo, katika awamu mbili za ujenzi.

Katika hatua ya kwanza ya ujenzi huo unatarajiwa kumalizika mwaka 2023, huku vitu vinavyotakiwa kujengwa ni Makazi, Barabara, Hospitali, Shule, Vituo vya polisi, Hoteli, Maduka makubwa, Kituo cha taka na Umeme wa jua.

Ujenzi wa awamu ya pili utaanza mwaka 2024 hadi 2029, kutajengwa na kutengenezwa vitu kama viwanja, hifadhi, vyuo vikuu, shule kubwa, hoteli, na sehemu ya soko kubwa la biashara.

Akon ni msanii anayefanya shughuli za kimuziki nchini Marekani ila kwao ni Senegal, na aliingia makubaliano mwezi Januari 2018 na Serikali ya nchini kwao, kuhusu maendeleo ya kujenga mji wake wa Akon City.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad