Ufaransa imepongeza mauaji ya kiongozi wa kundi la Al-Qaeda katika eneo la Afrika Kaskazini wakati wa operesheni dhidi ya kundi hilo linalofanya mashambulizi makali katika eneo la Sahel.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Florence Parly, amesema kuwa Abdelmalek Droukdel aliuawa na wanajeshi wa Ufaransa siku ya Alhamisi katika eneo la Kaskazini mwa Mali karibu na mpaka na Algeria ambapo kundi hilo lina ngome zake linalozitumia kufanya mashambulizi ya mabomu na utekaji nyara wa raia wa Magharibi.Parly aliitaja operesheni hiyo kuwa ya ''ufanisi mkubwa.''
Parly pia alitangaza kuwa mwezi uliopita, mwanachama mmoja mkuu wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu alikamatwa wakati wa mashambulizi mawili dhidi ya makundi ya itikadi kali.
Duru za jeshi la Ufaransa zinasema kuwa kifo cha Droukdel ambaye wakati mmoja alitajwa kuwa adui wa kwanza wa Algeria huenda kikaliacha kundi la Al-Qaeda katika eneo la kiislamu la Maghreb (AQIM) katika hali tata.
-DW
OPEN IN BROWSER