Uingereza yaitaka China kujizuia kuingilia mambo ya ndani ya Hong Kong





Uingereza imeitaka China kufikiria upya kuhusu kuongeza udhibiti wake juu ya Hong Kong, na kuheshimu majukumu yake kimataifa. Hilo linafuatia wasiwasi kwamba China inajaribu kukandamiza upinzani katika mji wa Hong Kong wenye mamlaka ya ndani. 

Akizungumza mapema leo, waziri wa mambo ya nje wa Uigereza Dominic Raab

amesema huu ni wakati muafaka kwa China kujizuia na kuheshimu uhuru wa Hong Kong kujiamulia mambo. 

Bunge la China ambalo ni kibaraka wa serikali limeidhinisha sheria ambayo inatoa mamlaka ya kulipuuza baraza la wawakilishi la Hong Kong, ambayo limesema inahitajika kupambana na ilichokiita ''ugaidi'' na ''kutaka kujitenga''. 

Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema inalenga kukandamiza uhuru wa kisiasa katika mji huo, na kuhujumu uhuru wake chini ya makubaliano ya mwaka 1997 baina ya Uingereza na China. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad