Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amemkaribisha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mwanachama wa CCM Bernard Membe, kuunganishe nguvu kupitia vyama mbadala hii ni mara baada ya yeye kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.
Kushoto ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na kulia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter wa chama hicho hii leo Juni 30, 2020, ambapo imeandikwa hivi,
“Ndugu yangu Bernard Membe kafukuzwa uanachama wa CCM, ninajua bado anatetea haki yake ya uanachama huko ni hatua sahihi, hata hivyo muda wa kuleta mabadiliko katika nchi umewadia, ninamsihi afanye maamuzi ya kuunganisha nguvu kupitia vyama mbadala” umeeleza ujumbe huo ambao umetolewa na Zitto Kabwe.
"Mimi najua @BenMembe anaipenda Tanzania na ni Mwana demokrasia.
Adhihirishe mapenzi yake kwa nchi yetu kwa kuongeza nguvu kwa vyama mbadala."@zittokabwe
Kiongozi wa Chama pic.twitter.com/kD6E7XHTDS
— ACT Wazalendo (@ACTwazalendo) June 30, 2020
OPEN IN BROWSER
Wewe Dogo, Si uliwahi kuwaga Mbunge
ReplyDeletekipindi kilichopita?
Sasa ya watu Unayatakia nini?
Mbona una kihere here. wewe umeshapita
wakati wako. Tulia huko huko twita
kabla ya Rahisi wa Online hajakustukia
Mdau, huyu ana Hulka ya uchonganishi
DeleteYa Membe mwachie Membe.
Wewe yanakusshia nini? au hujui
kwamba Kibajaji anajua kukuna.
Bernard Camilius Membe, Unanishangaza na kunihuzunisha Mwanagu.
ReplyDeleteHivyo wewe umeshindwa kusoma alama za Nyakati?
Leo ulete fikira ya CUF Lipumba aungane na Maalimu Seif kweli jameni? inakuingia Akilini!!
Au Mbatia aungane na Mbowe.. Faru Joni ni kitu kisichowezekana.
kwa hali halisi ilivyo sasa. Au mie Sielewi? Nijuze mwanangu.
Nisicho kielewa zaidi ni Upeo wa Akili zako. kwamba wakiungana labda wewe ndio Ugombee.. Unataka kugombe NINI?
Kwa huu muonekano wa Fikra Zako.. inaelekea hata Ujumbe wa nyumba kumi kumi HUUWEZI na pia inanitia Mashaka kwamba wewe ulisha wahi kuwa nasikia WAZIRI.. Kweli WAZIRI.. Hasa WAZIRI..??
Inatia shaka zaidi alie kuchagua KILAZA wewe kukupa Madaraka.
Mie ningekushauri , Kutamana na VIBEKO , Mpange mikakati yenu
mtakayo kubaliana kuanzisha Saccozi mpya ya Boda Boda au Car washing frenchasing Business na wewe uwe Raisi wa Saccozi hiyo
mpya. na ukitaka ushauri zaidi tafadhali umuone Mr, Steve Nyerere
ili aweze kukusaidia on How to Deal with Vibeko.
Hivyo uko Tanzania au Nchini Twita ..? Manake fikra zako haziingi Akilini ni kama za Kilaza wa Kigoma.
Nakutakia mafanikio mema katika Biashara yako Mpya. Tujulishe ukisha Sajili ili tukusapoti kama Kawa Mwanangu. Siasa Huijui.