Ukiona Haya, Fahamu Muda wa Kubadilisha Betri la Simu yako Umefika!

Ingawa betri la simu limetengenezwa na uwezo wa kuchajiwa mara kwa mara ila inafika muda ambao lazima libadilishwe tuu. Hasa inategemea utumiaji na utunzaji wa betri husika ila mara nyingi betri linaweza kuwa zima kabisa kati ya miezi 6 hadi miaka miwili ya kutumiwa.

Haya ndiyo ya kuangalia ili kutambua muda wa kubadilisha betri lako.

1.Muda wa betri kukaa na chaji umepungua na ata zaidi ya nusu ya mwanzo
Itakapofika muda ambao kiwango cha kupoteza chaji kimepungua kufikia hadi nusu au chini zaidi ukilinganisha na mwanzoni ulipoinunua kwa mara ya kwanza basi ujue haifai tena.

Muda mwingine utakuta simu inaonesha inakiwango cha asilimia nyingi tuu ya chaji alafu ghafla unashtukia imezima, ukiwasha inasema ‘battery low’, badilisha tuu betri.

Betri lisilofanya kazi kwa ufanisi linaathiri ata vitu vingine kwenye simu yako.

2. Simu inapata joto sana
Je unasikia simu inakuwa yamoto sana hasa hasa joto hilo likitokea eneo la betri? Epuka hatari, badili betri mara moja. Pia mara nyingi ikitokea hivi kwa simu utagundua pia ata betri halikai na chaji sana ukilinganisha na zamani.

3. Linachukua muda mrefu zaidi kujaa
Betri linatakiwa kuchukua masaa machache tuu kujaa, mara nyingi kwa simu za kisasa ni kati ya dakika 30 hadi masaa mawili hivi.

Ukiona kuna tofauti ya masaa kadhaa ukilinganisha na lilivyokuwa zamani basi ujue tayari ndani mwake mambo hayaposawa na hivyo uanze maandalizi ya kununua jipya kuepusha usumbufu wa kuchaji kwa muda mrefu kitu ambacho ni hatari.

4. Umbo limebadilika: Kuvimba
Hili jambo maarufu kwa watu wengi. Betri zuri si kwa simu ata bali ata kwenye magari, ni betri ambalo pande zote zimenyooka.

Kuonesha uvimbe katika pande yeyote ni dalili ya kwamba betri limeshachoka…yaani limetumika sana au limewekwa katika mazingira mabovu. Ukiona hivi ufanye haraka kununua jipya kwani betri lililovimba huwa na hatari ya kupata milipuko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad