Kuna wakati umekuwa ukujiuliza sana kwa nini wewe ni maskini na kwa nini wengine ni matajiri, labda nikwambie tu hivi, usiendelee kujiuliza swali kama hili ngoja tu ni kupe jibu la moja kwamba, umaskini au utajiri unaanzia kwenye akili yako.
Kile unachokifikiria sana kwa muda mrefu bila kujali unafikiria umaskini au utajiri hicho ndicho utakachokipata. Hauzuiliwi kufikiria na kutenda kitajiri hata kama pato lako ni dogo au hata kama unajiona ni maskini, lakini tambua chanzo cha umaskini au utajiri ni akili yako.
Kwa hiyo kwa mfano unajiona umepigika, huna pesa mfukoni na umejikuta umekuwa ni mtu wa kukopa huku mara kule, hiyo ni dalili tosha kwamba pia ni matokeo ya akili yako iliyopigika ama akili ya kimaskini ambayo umewekeza kwa muda mrefu.
Kama upo katika hali hii, haina haja ya kujichukia au kujiona hovyo hovyo kubali kujirekebisha na kuchukua hatua zitakazokuwezesha kusonga mbele kimafanikio. Ukiwa mbishi, nikupe uhakika huu utaendelea kuteseka na umaskini.
Kwa hiyo unatakiwa uangalie na kujua kwamba kinachokufanya uendelee kuwa maskini sio kwa sababu huna pesa au huna mtaji, bali ni kwa sababu ya matokeo ya mfumo wa mawazo yako ulionao na umeujenga kwa muda mrefu.
Dawa pekee ya kuweza kukata mizizi ya umaskini ni kwa wewe kuamua kubadili mfumo wa mawazo ambayo unayo ya kimaskni na kujenga mfumo mzuri chanya utakao kuwezesha kukusaidia kufanikiwa.
Chanzo cha utajiri na umaskini wowote ule ni matokeo ya mawazo yako. Matokeo ya mawazo yako yanakuja na kile unachojifunza na kukiweka mara kwa mara akilini mwako,
hicho ndicho kinachoonekana kwa nje.
Ni wapi unatakiwa kuanzia ile ufutilie mbali historia ya umaskini?
1. Jifunze kila siku kuhusu mafanikio kwa kutafuta kanuni na mbinu mbalimbali zitakazokuwezesha kufanikiwa kupitia vitabu au semina.
2. Kaa na watu wenye mafanikio kwa pamoja. Jifunze kwao. Acha kung’ang’ania kuwa na watu ambao hata wewe hawana uwezo wa kukusaidia chochote.
Njia sahihi ya kukufanya wewe ukafanikiwa na kuwa na mawazo sahihi. Yatafute mawazo hayo sahihi kila siku ya maisha yako na uwe miongoni mwa watu wenye mafaniko makubwa.