Vitisho Wanavyopokea Wasomali Wasioamini Kwamba Mungu yuko



Raia wa Kisomali wasioamini kwamba kuna kuna Mungu wanaoishi ughaibuni wana kundi lao katika mtandao wa Facebook linalopinga imani za raia wa Kisomali ambao ni Waislamu lakini mara huwa wanapokea vitisho vya vifo, amesema wanahabari Layla Mahmood.

"Mimi nitakuua. Nitakutafuta. Na nitakata kichwa chako," ni moja ya vitisho alivyopokea Ayaanle, raia wa Kisomali asiyeamini Mungu ambaye anaishi Canada.

"[Lakini] hali kama hiyo ni kawaida," mwasisi wa ukurusa wa Somali Freedom Page anasema hivyo anapozungumzia vitisho anavyopokea kupitia simu yake.

Kundi hilo maarufu kwenye mtandao wa Facebook, ambalo lina watu zaidi ya 80,000 linaongozwa na waliokuwa Waislamu ambao kwa sasa wamebadilika na kuwa wasioamini Mungu kama wanavyojiita wenyewe.



Awali, kundi hill liliundwa ili kutengeneza mazingira ya kujadili masuala ya kidini lakini sasa linaendeleza uhuru wa kujieleza kwa raia wa Kiislamu ambao wanahisi kutengwa na jamii inayozingatia utamaduni wa Kisomali.

Ayaanle hakutaka kutoa majina yake kamili wakati anaelezea shughuli za kundi lao.

Karibia mwaka 2016, alikutana na kundi hilo la Wasomali katika mtandao wa Facebook ambalo lilionekana kutengeneza mazingira ya kuzungumzia mijadala kwa uwazi.

"Nikaanza kuchangia mijadala kuhusu dini na kila mmoja akaanza kuchangia mjadala huo kwa nguvu yake yote. Wakabadilika na kuwa kama makombora jinsi wanavyorusha maneno makali. Wakanifanya nihisi kama mtu ambaye nimetekeleza mauaji."

Akaondolewa taratibu kwenye kundi hilo jambo la kawaida kwa wale wenye kuwa na maoni tofauti katika mijadala ya haina hii kwa majukwaa ya mtandao ya kijamii ya Wasomali.

Ayaanle akahisi kwamba njia pekee ya kutatua changamoto hiyo ilikuwa ni kufungua ukurasa mpya wa majadiliano kwa uhuru litakalokuwa na sheria mpya.

"Nilitaka kuwa na mtandao ambao watu wangejadili kwa uhuru kila wanachopenda."

Kilichompa Ayaanle msukumo ni imani ya kwamba majadiliano ya Wasomali wa sasa kuhusu dini yamekuwa na masharti mengi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu.

"Uislamu haubadiliki. Huwezi kuikosoa dini hiyo au kusema lolote kuhusu Uislamu.

"Kwa sasa hivi vijana wanabadilika, wanaweza kuvumilia kidogo katika mijadala na kukosolewa.

"[Lakini] wengi wa walio kulia nchini Somalia na kwenda nchi za Magharini baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe wazo la ikiwa atakubali mtu kukosoa Uislamu kwao adhabu ya mtu huyo ni kuuawa. Wanafikiria kwamba hatua hiyo ni haki yao. "

Na hiyo ndio sababu amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa.

"Hayo ni baadhi ya yale ambayo ninataka kuyaweka kwenye ukurasa wa mtandaoni - kuonesha kwamba Uislamu sio kuwa ni dini ambayo haikosolewi. Pia nayo inaweza kukosolewa. Inaweza kujadiliwa na inaweza kuzungumziwa kwa uwazi."



Nchini Somalia, na katika jimbo la Somaliland, kukufuru au kukashifu dini ni kosa ambalo mtu anastahili kufungwa na mtandao alioufungua Ayaanle umekabiliana na changamoto hiyo.

Kundi hilo lilifanya kampeni na kuchangisha pesa za msomi Mahmoud Jama Ahmed-Hamdi. Alikuwa mhariri wa chuo kikuu ambaye alikamatwa kwa kuandika kwenye mtandao wa Facebook ujumbe ambao unahoji uhalali wa kumuomba Mungu kama njia ya kukabiliana na kiangazi mwaka 2019.

Alihudumia kifungo cha miezi 10 kabla ya kutolewa kwa msamaha wa rais lakini bado yuko katika hatari ya kushambuliwa na makundi yenye msimamo mkali. Imam mmoja mashuhuri alitoa wito wa kuuawa kwake.

Tukio hilo linaonesha nguvu ya madaraka nchini Somalia na Somaliland, huku kukiwa na sintofahamu kati ya msimamo wa viongozi wa kidini na serikali

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad