Kufautia mauaji ya mmarekeani mwenye asili ya Afrika aliofariki mikononi mwa Polisi Mei 25 nchini Marekani, maandamano makubwa yamefanyika katika miji tofuati ulimwenguni, maandamnao ambayo yamekemea ubaguzi wa rangi na matumizi ya nguvu zilizokithiri hadi kupelekea maafa.
Maandamano hayo yamepelekea waandamanaji kung oa kila ambacho ni ishara ya ubaguzi wa rangi katika Historia .
Moja ya ishara hizo ambazo zimeshambuliwa na waaandamani ni sanamu la mfanyabiashara mkubwa wa watumwa nchini Uingereza Bristol, nchini Ubelgiji sanamu la mfalme wa zamani wa taifa hilo Leopold wa Pili limengolewa na waandamanaji huku wito ukiendelea kutolewa kuondoa masanamu hayo katika ardhi ya Ubelgiji.
Leopold wa Pili, ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa mali yake binafsi na kulinga na nyaraka za historia zinaonesha kwa ushahidi uhalifu na matendo ya kinyama yalioendeshwa na uongozi wa ufalme huyo wakati wa ukoloni JK Kongo.
Waandamanaji mjini Brussels walikuwa na mabango wakikemea serikali kuacha sanamu la mtu kama huyo ambae ameua watu zaidi ya milioni 15 na kukumbusha kuwa uhaia wa mtu mweusi pia una thamani.
Muamko huo ni baada ya kuuawa kwa George Floyd nchini Marekani.
Sanamu la Leopold wa Pili limechomwa moto wiki ilipita na mabaki yake tayari yameondolewa mkoani Anvers.