Wabunge 69 wa CHADEMA Kuhojiwa Leo na Takururu.....
2
June 10, 2020
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Makao makuu Dodoma, leo inatarajia kuanza kuwahoji Wabunge na waliokuwa Wabunge wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAKUKURU inasema wabunge hao watahojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali ambazo zimetolewa na baadhi ya wabunge ambao wamehama chama hicho na kudai kuna fedha walikuwa wakichangishwa lakini matumizi yake hayajulikani.
"Tunapenda kuthibitishia umma kwamba ni kweli kuwa TAKUKURU Makao makuu imewaita waheshimiwa wabunge wa CHADEMA na waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho kwa mahojiano" imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inasema mahojiano hayo ni mwendelezo wa uchunguzi unaoendeshwa na TAKUKURU Makao makuu wa malalamiko dhidi ya matumizi ya fedha za chama na hatua ya Sasa ni kuhoji wabunge sitini na tisa(69).
Kwa mujibu wa malalamiko hayo wabunge hao wanadai walikuwa wakikatwa kwa wabunge viti maalumu walikuwa wakikatwa kiasi Cha milioni moja laki tano na sitini(1,560,000) na wabunge wa kuchaguliwa walikuwa wakikatwa laki tano na ishirini (520,000).
Na wabunge hao walidai kutojua matumizi ya fedha hizo, na kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenarali John Mbungo, Mei 27, 2020 kwamba uchunguzi tayari ulishaanza na baadhi ya viongozi wameshahojiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU yataanza kufanyika leo TAKUKURU Makao Mkuu Dodoma na yanatarajiwa kukamilika wiki ijayo
Tags
Wame dhulumiwa vya KUTOSHA.
ReplyDeleteWame dhalilishwa vya KUTOSHA.
Wame Ibiwa vya KUTOSHA.
Wame Danganywa toto vya KUTOSHA.
Wame Gawanywa vyo KUTOSHA.
Wametumika kujenga na kupandikiza chuki na kupinga kila jambola Serikali
iliyo madarkani awamu zote vya KUTOSHA
Mbongo na timu yako Mahiri Tunaimani.
haki itafikiwa na kupatikana.
Mahoteli ya kitalii kwa pesa hizi na
uufuaji wa pesa ulioendelea utabainika
na wanufaika kullikana na njia danganyifu (Njia Hewa) katika kufaikisha sualazimala Uporaji huu.
Wame dhulumiwa vya KUTOSHA.
ReplyDeleteWame dhalilishwa vya KUTOSHA.
Wame Ibiwa vya KUTOSHA.
Wame Danganywa toto vya KUTOSHA.
Wame Gawanywa vyo KUTOSHA.
Wametumika kujenga na kupandikiza chuki na kupinga kila jambola Serikali
iliyo madarkani awamu zote vya KUTOSHA
Mbongo na timu yako Mahiri Tunaimani.
haki itafikiwa na kupatikana.
Mahoteli ya kitalii kwa pesa hizi na
uufuaji wa pesa ulioendelea utabainika
na wanufaika kullikana na njia danganyifu (Njia Hewa) katika kufaikisha sualazimala Uporaji huu.