Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Wabunge wa chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, wameendelea kuhojiwa na taasisi ya kuzuia ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Makao Makuu Dodoma juu ya matumizi mabaya ya fedha za michango ya wabunge wa chama hicho.
Mwendelezo wa mahojiano hayo yanafanya kufikia idadi ya wabunge wa chama hicho waliohojiwa kufikia 43 ambapo lengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa imetaka kujua matumizi ya fedha ambazo zimekuwa zikichangwa na wabunge hao.
Hivi karibuni baadhi wabunge wa CHADEMA kwa wakati tofauti walitangaza kukihama chama hicho kwa madai ya kuchangishwa fedha lakini tutojua namna fedha hizo zinavyotumika huku wengine wakidai kunyanyaswa kingono.
Baadhi ya wabunge waliohojiwa siku ya leo ni Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema, Mbunge wa Tarime vijijini John Heche, Sophia Mwakagenda, Cesilia Pareso, Mariam Msabaha.
Wengine ni Joyce Sokombi, Susan Masele, Anna Gidalia, Zainabu Bakari, Conchesta Lwamlaza, Grace Tendega, Sabrina Sungura, Lucy Mageleli, Lucy Owenya, Joseph Makumbi.
Zoezi la kuwahoji wabunge hao litaendelea siku ya jumatatu ili kutimia kwa wabunge sitini na tisa wanaotarajiwa kuhojiwa na taasisi hiyo.
Wame Ibiwa vya KUTOSHA.
ReplyDeleteWame Danganywa toto vya KUTOSHA.
Wame dhulumiwa vya KUTOSHA.
Wame dhalilishwa vya KUTOSHA.
Wame Gawanywa vya KUTOSHA.
Wametumika kujenga na kupandikiza chuki na kupinga kila jambo la Serikali
iliyo madarkani awamu zote vya KUTOSHA
Mbongo na timu yako Mahiri Tunaimani.
haki itafikiwa na kupatikana.
Mahoteli ya kitalii kwa pesa hizi na
uufuaji wa pesa ulioendelea utabainika
na wanufaika kujulikana, na njia danganyifu (Njia Hewa) katika kufaikisha suala zima la Uporaji huu.
Mbaya Zaidi..!!Ame bambikiza Madeni Hewa
ReplyDeletekwa Chama akidai, alikikopesha katika Mchakato wa Uchaguzi 2015. Kupitia Halmashauri kuu ya Kamati Kuu???
MADENI HEWA YA KIPORAJI NA KUPELEKA KWA SHEMEJI AMBAE ANAZIRUDISHA KWA MLENGWA.!
MPAKA LINI ????