Chelsea hii leo siku ya Jumanne imefuata nyayo za Liverpool kuwa miongoni mwa klabu zinazotoka Premier League kupiga goti moja kama ishara ya kuunga mkono harakati za ‘Black Lives Matter’ kupinga ubaguzi wa rangi kufuatua kifo cha Mmarekani mwenye asili ya watu weusi, George Floyd.
Chelsea players took the knee in the H formation for 'human' during training on Tuesday
Wachezaji kutoka katika klabu ya jiji la London wamepiga magoti wakati wa mazoezi katika viwanja vya Cobham.
Mlindalango, Kepa ameelezea katika akaunti yake ya twitter kwa kuandika ujumbe kuwa inatosha, ”Inatosha, sisi sote ni binadamu. Pamoja tupo imara.”
Newcastle's players also delivered a statement of their own as shared on Twitter
Wachezaji wa klabu ya Newcastle wakiwa wamepiga magoti katika kuunga mkono harakati za ubaguzi.
Hapo jana Jumatatu kikosi cha Liverpool kilipiga magoti kwa kuonyesha ishara ya umoja juu ya kifo cha Mmarekani mweusi aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi kabla ya kuanza mazoezi yake katika uwanja wa Anfield.
The Liverpool squad stopped training to show solidarity with the Black Lives Matter movement
Wachezaji hao kila mmoja alikunja goti moja na kutengeneza duara katikati ya uwanja na kuitazama kamera iliyokuwa ikiwamwilika uwanjani hapo.
Nyota hao wameonekana kuvalia jezi zenye rangi tofauti tofauti, wengine wakiwa na rangi nyeusi, nyeupe, nyekundu wakati wengine wakiwa wamevalia jezi za mazoezi.
Hayo ni mazoezi ya kwanza kwa kikosi cha kocha Jurgen Klopp katika dimba la Anfield tangu kusimama kwa michezo kufuatia kusambaa kwa virusi vya corona.