Wadau Watoa Maoni Kuelekea Kwenye Mabadiliko Young Africans



Kuelekea kwenye mabadiliji ya Young Africans, Mwenyekiti wa klabu hiyo Dk Mshindo Msolla alisema wawakilishi wa matawi kutoka kila pande za Tanzania watapata mafunzo maalumu jijini Dar es Salaam na kupewa makabrasha ambayo watayatumia kuendesha elimu ya mabadiliko hayo pindi watakaporejea kwenye matawi yao.

“Gharama hizi za awali, zitakuwa chini ya GSM ambayo imejitolea na hatutalazimika kumlipa chochote. GSM kama mdhamini, imekuwa mstari wa mbele kuona klabu yetu inafanikiwa katika kila idara,” alisema Dk Msolla.

Hersi Said, ambaye ni mkurugenzi wa uwekezaji GSM alisema watasaidia mchakato huo ili Yanga ijitegemee na kuondokana na hali iliyo nayo sasa.

“Huwezi kuingia mkataba na kuwekeza kwenye kampuni ambayo unajua haitaweza kukufikisha pale ambapo unataka kufika.

 Mgongolwa alisema hatua waliyofikia inaleta matumaini ya mafanikio katika mchakato huo.
 “Tumekuwa tukipokea simu zaidi ya 300 kwa siku, wote hao wamekuwa wakitoa maoni kuhusiana na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, tumewasilikiza na tunasubiri kupata mapendekezo ya La Liga na kufanya majumuisho ya pamoja na kamati ya utendaji wa Yanga kabla ya kutoa taarifa rasmi kuwa mfupo upi unafaa.”

 Naye mkurugenzi wa Biashara wa Kimataifa wa La Liga, Juan Botella alisema wamefurahi kuingia mkataba na Yanga ambayo inakuwa ya kwanza katika Ukanda wa Afrika kufanya hivyo.

Botella alisema kuwa kampuni yao ina wataalam wa kimataifa ambao watashirikiana na klabu ya Sevilla ili kuhakikisha Yanga inakuwa na mfumo wa kisasa wa uendeshaji na kupata mafanikio.

Kwa upande wa mkurugenzi wa Kimataifa wa Masoko na Biashara wa Sevilla, Oscar Mayo alisema makubaliano yao na Yanga yanalenga kuleta maendeleo katika nyanja za ufundi, masoko na uongozi, huku rais wa klabu hiyo Jose Castro Carmona akisema anaamini Yanga itafanikiwa na kuwa ya mfano Tanzania na Afrika.

 Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alipongeza hatua ya Yanga kuelekea kwenye mabadiliko huku akikumbushia majaribio mengine mawili yaliyoshindikana kwenye mabadiliko.

Kikwete alisema Yanga ilianza mabadiliko enzi za uongozi wa katibu kkuu, George Mpondela (marehemu) na baadaye Tarimba Abasi pia Manji ila awakufanikiwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad