Waganga wa Tiba asili wakubali kusajili nyara wanazomiliki



Waganga wa tiba asili zaidi ya 300, Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wamekubali kusajili nyara za Serikali wanazomiliki kama sehemu ya vitendea kazi vyao ikiwemo ngozi mbalimbali za Wanyama, ili kuweza kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu za nchi zinavyoelekeza, na kuwabaini wale wachache wasiotaka kufuata maelekezo ya Serikali katika utendaji wao wa kazi.

Hatua hiyo imekuja, baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga kutoa mwezi mmoja kwa waganga hao kuhakikisha kuwa wanasajili nyara za Serikali wanazomiliki ili kuwaondoa waganga matapeli na wasio taka kufuata taratibu na sheria za nchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad