Wahamiaji Waanza Tena Kumiminika Ulaya Baada ya Corona



Wimbi la wahamiaji kuelekea barani Ulaya limeanza tena upya kufuatia kupunguwa sana kutokana na janga la virusi vya korona.

Kwa mujibu wa wakala wa mipaka ya Umoja wa Ulaya, Frontex, idadi ya watu wanaowania kuingia Ulaya kwa njia haramu ilishuka sana mwezi Aprili na kufikia hadi 900, lakini mwezi uliomalizika wa Mei umeshuhudia idadi hiyo ikipanda hadi 4,300. Idadi ya mwezi Aprili inatajwa kuwa ya chini kabisa tangu Frontex ilipoanza kusajili idadi ya wahamiaaji mwaka 2009.

Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu wa 2020, watu 31,600 walisajiliwa kujaribu kuvuka mipaka kuingia Ulaya, ikiwa ni anguko la asilimia 6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mediterenia ya Mashariki imeendelea kuwa njia kuu ya wahamiaji hao kujaribu bahati yao ya kuingia Ulaya, ambapo wahamiaji 1,250 wengi wao kutokea Afghanistan walipitia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad