"Wanafunzi Wakisimama Msikamate Gari" - Paul Makonda


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaambia Askari wa Usalama Barabarani kwamba, wakiona Daladala imesimamisha abiria ambao si wanafunzi kwa kipindi hiki waikamate kwa kuwa agizo la 'level seat' bado halijatenguliwa.


Makonda ameyabainisha hayo leo Juni 2, 2020 wakati akitoa ruhusa kwa madereva na makondakta wa daladala, kuhakikisha wanasimamisha wanafunzi ambao hawatozidi wanne, kwa kuwa wao hawana uwezo wa kulipia nauli yote na kwa kufanya hivyo watawawezesha kuwahi mashuleni kwao.

"Suala la level seat lipo pale pale wazingatie, lakini wanapokuja kwenye point ya wanafunzi hawana sababu ya kumuacha kwa sababu hana pesa ya kulipa kama mtu mzima, wanafunzi wanne wakisimama ndani ya daladala si dhambi, kwahiyo Traffic mlioko barabarani mkikuta gari limebeba wanafunzi wamesimama wanne msilikamate ila mkikuta limesimamisha abiria kamateni hiyo ni halali yake" amesema Makonda.

Makonda amesema kuwa suala la kusimamisha wanafunzi wanne ndani ya daladala linaanza rasmi leo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Naamini shida ya usafiri dar ingepungua sana endapo kungekuwa na mwendo kasi za kutosha
    Idea ya mwendo kasi ni bora tu kama mabus ni mengi. Ingekuwa kila baada ya angalau dk 8 mtu unapata bus. Lakini mtu unakaa weee bila kuona bus na likija ni kugombea na ndani watu kibao. Ungeboresha mwendokasi, lete mabus mengi ya kutosha. Lete na reli hadi mbagala chamazi. Mabasi ya abiria yawe makubwa, madogo madogo yanaleta wingi wa msongamano na shoo ya mji ingepungua. Bodaboda mjini! Labda kwa muda tu tumisubiria mkakati wa kudumu. Mji ukipendeza sana bila bodaboda. Sasa shoo ya mji itarudia kupoteza hadhi au muonekano mzuri wa jiji. Ile meli ya bagamoyo ipo wapi? Zitafutwe speed boti kama zile za zanzibar angalau 6 zifanye safari Kati ya kivukoni bagamoyo. Mbona siyo ngumu kupunguza msongamano? Silioni km tatizo, naliona linatatulika kabisa. Inahitaji tu resources ambazo tayari tunazo (pesa) na management bobezi zilizo nzuri. Makonda unda tume. Km alibyofanya Umy, tume ya wabobezi. Dar inabidi ipendeze kwa sura pia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad