Watoto na Tiketi Feki Wavuruga Kampeni ya Trump


Rais wa Marekani, Donald Trump amefanya kampeni yake ya kwanza tangu kuanza kwa mlipuko wa virusi vya Corona ambapo watu wachache wamejitokeza.

Vijana wadogo wanasemekana kuwa walijiandikisha kununua tiketi wakiwa na nia ya kutohudhuria mkutano huo kwa lengo la kuhakikisha viti vinabaki tupu katika mkutano huo, lakini kikosi cha kampeni cha 2020 cha Trump 2020 kimesema kuwa kilikua kimeondoa tiketi hizo feki.

Awali, Rais Trump alisema watu takriban Milioni 1 wamenunua tiketi za kampeni hiyo iliyofanyika Tusla, Oklahoma lakini uwanja unaomudu watu takriban 19,000 umeonekana ukiwa na watu wachache.

Mkurugenzi wa kikosi cha kampeni ya Trump amesema katika taarifa aliyoitoa kuwa “maombi ya tiketi za simu hatukuyafikiria” kwani tuliwapokea watu kwa misingi ya yule anayefika ndiye anayehudumiwa kwanza .

Brad Parscale amevilaumu vyombo vya habari na waandamanaji kwa kuzishawishi familia zisihudhurie kampeni hiyo.

Trump alizungumza kwa takriban saa mbili na kuwaita waliokuwepo uwanjani hapo mashujaa. Amevitupia lawama pia vyombo vya habari na waandamanaji akisema wamesababisha wanaomuunga mkono wasihudhurie
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad