Waziri mkuu wa Uingereza awaonya watu kutohudhuria maandamano



Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo amewashauri watu kutoshiriki katika maandamano ya mwishoni mwa wiki hii na kusema yeyote atakayeharibu mali ya umma ama kuwashambulia polisi atakabiliwa kikamilifu kisheria. 

Johnson amekiambia kituo cha utangazaji cha nchini humo cha Sky News kuwa ujumbe wake kwa kila mtu ni kwamba hawapaswi kuandamana kwa sababu yoyote ile. 

Amesema polisi watawakamata watu zaidi na kuhusishwa na maandamano ya awali. 

Johnson ameongeza kuwa kushambuliwa kwa polisi hakuruhusiwi nchini humo na njama zilizopangwa za kuharibu mali ya umma pia hazitakubalika. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad