Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani asema Maandamano ya Marekani ni zaidi ya halali



Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amesema maandamano ya kupinga ukatili wa polisi nchini Marekani ni zaidi ya halali, na kwamba ana matumaini yatazusha mabadiliko. 

 Ameeleza matumaini yake kuwa maandamano ya amani hayawezi kugeuka kuwa ya ghasia, na kwamba hata zaidi ,kuna matumaini yataleta athari nzuri. 

 Maas ametoa wito wa uhuru wa vyombo vya habari kwa waandishi wanaotoa maelezo kuhusu maandamano hayo, akisema serikali ya Ujerumani itawasiliana na maafisa nchini Marekni kuunga mkono mwandishi wa DW ambaye alishambuliwa kwa risasi na kuzuiwa kufanyakazi yake. 

Ghasia zozote zinazotokea katika muktadha huu sio tu zinapaswa kushutumiwa, juu ya yote zinapaswa kufanyiwa uchunguzi ili waandishi waweze kulindwa wakati wakifanyakazi zao, Maas alisema. 

Stefan Simons wa DW alishambuliwa kwa risasi na polisi katika matukio mawili tofauti wakati akitangaza maandamano ya mjini Minneapolis. 

Alikuwa amevaa koti lililoandikwa chombo cha habari, Press katika matukio yote mawili na alijitambulisha kama mwandishi habari.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad