Waziri Waitara "Siumwi Corona ila ni Mgonjwa Nimelazwa Dodoma"



Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa ni kweli anaumwa na amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma na kwamba haumwi Corona kama ambavyo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Waitara ameyabainisha hayo leo Juni 15, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kusema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri kwani hapo awali alikuwa hawezi hata kupokea simu.

"Kuuumwa naumwa na nimelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, kusema naumwa nini sijui kwa sababu sijapata taarifa ya wataalam, kwahiyo aliyeandika mnaweza kumhoji akawaambia aliongea na mamlaka zipi, lakini mimi taarifa za Corona sina" amesema Naibu Waziri Waitara.

"Hali yangu haikuwa nzuri sana ila kuanzia jana nimeanza ku-improve, kabla ya hapo nilikuwa siwezi hata kuongea na simu,  nipo hospitali karibia wiki sasa,  naumwa tu kawaida kwani tangu nimekuwa Naibu Waziri nimezunguka sana sijawahi kupumzika wala kuchukua likizo" amesisitiza.

Waitara ameongeza kuwa amekuwa akisikia taarifa za yeye kuumwa kupitia mitandao ya kijamii, lakini yeye ameamua kupuuzia ila kwa yeyote anayetaka kujua hali yake basi aende Hospitali aliyolazwa ama awasiliane naye.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad