WhatsApp Wazindua Huduma ya Kupokea na Kutuma Pesa


Baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo na majaribio, mtandao wa WhatsApp umezindua huduma ya malipo kupitia programu tumishi hiyo.

Mtandao huo wa kutumiana ujumbe unaomilikiwa na Facebook umetangaza kuwa watumiaji wake wa Brazil ndio walioanza kutumia huduma hiyo ya kutuma na kupokea fedha kwa kutumia Facebook Pay, huduma ya malipo ambayo Facebook iliizindua mwaka 2019.

WhatsApp imesema kuwa huduma hiyo ya ni bure kwa watumiaji wa kawaida, lakini wanaotumia kwa masuala ya biashara watalipa ada 3.99% kupokea malipo na itahitaji tarakimu sita (PIN) au alama za kidole kukamilisha muamala.

Kwa nchini Brazil ambapo majaribio yameanza, watumiaji wanatakiwa kuunganisha WhatsApp zao na Visa, Mastercard credit au debit card pamoja na watoa huduma wa ndani (nchini humo) ambao ni Banco do Brasil, Nubank na Sicredi ili kukamilisha miamala.

Taarifa hiyo imekuja kwa kushtukiza kwani kwa muda sasa WhatsApp imekuwa ikifanya majaribio ya huduma ya malipo nchini India kwa kutumia UPI badala ya Facebook Pay.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad