WHO: Virusi Vinarejea Tena Barani Ulaya



Bara la Ulaya limeshuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 tangu nchi hizo zilipoanza kulegeza vizuwizi vyenye lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi hatari vya corona, shirika la afya ulimwenguni limesema leo.

Wiki iliyopita, Ulaya ilishuhudia ongezeko la kila wiki la kesi za maambukizi kwa mara ya kwanza katika muda wa miezi kadhaa, mkurugenzi wa kanda ya Ulaya wa WHO Hans Kluge aliwaambia waandishi habari.

Amesema zaidi ya nchi 24 barani Ulaya zimeshuhudia ongezeko la virusi hivyo hatari. Ameonya kwamba katika 11 kati ya nchi hizo, ongezeko kubwa la maambukizi limesababisha kuzuka tena kwa usambaaji ambao kama hautashughulikiwa utasababisha mifumo ya huduma za afya kuwa katika ukingo wa kushindwa tena barani Ulaya.

Kluge hata hivyo hakuzitaja nchi hizo, ama kutoa idadi maalum ya maambukizi.

Ujerumani ilianza kulegeza vizuwizi kiasi ya wiki saba zilizopita na nchi hiyo imeathirika zaidi na imeweka vizuwizi tena kwa zaidi ya watu 600,000 katika wilaya mbili za nchi hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad