Wito wa kaka wa George Floyd kwa baraza la seneti Marekani



Kaka wa mmarekani mwenye asili ya Afrika  George Floyd atoa wito  wa marekebesho katika jeshi la Polisi nchini Marekani. 

Siku moja ya baada ya kuzikwa ndugu yake George Floyd  baada ya kukandamizwa shingoni kwa goti na afisa wa jeshi la Polisi Minneapolis, kaka wa muhanga huyo  Philonise Floyd ametolea wito baraza la seneti la Marekani kufanya mabadiliko na kuepusha maafa kama ilivyotokea kwa ndugu yake George Floyd Mei 24. 

Philonise Floyd amesema kwamba  haki kwa George Floyd itendeke na ndilo jambo ambalo linasubiriwa na watu wote walioandamana kukemea tukio hilo. 

Nchini Marekani  robo ya watu wanaouawa mikononi mwa Polisi ni watu wenye asili ya Afrika , jamii ambayo ni asilimia  13 ya raia wote wa Marekani. 

Ndugu huyo wa George Floyd ameshiriki katika  mkutano wa wawakilishi uliofanyika kwa ajili ya kujadili mustakabali wa kufuatwa kuhusu matumizi ya nguvu kwa maafisa wa usalama wanapokuwa katika kutimiza wajibu wao. 

Katika hotuba yake iliokuwa na ujumbe mzito dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani, Philonise Floyd amesema kuwa aliguswa mno na video iliochukuliwa na shahidi wa tukio lililopelekea kuuawa kwa ndugu yake. 

George Floyd aliwasihi maafisa wa usalama waliokuwa wamemkamata akiwaomba wamuache angalua aweze kupumua bila ya kusikilizwa hadi kupelekea kifo chake. 

Kifo cha George Floyd kimepelekea maandamano makubwa nchini Marekani  na kung olewa  kwa masanamu ya viongozi wa kihistoria ambao wanatambulika vema kwa matendo yao ya kibaguzi  na biashara ya utumwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad