Yafahamu mambo muhimu kutoka kwenye bajeti ya serikali 2020/21



 
1. Jumla ya shilingi trilioni 34.88 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21. Mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya halmashauri) yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 24.07, sawa na asilimia 69.0 ya bajeti yote.


2.Kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini;

Kufuta tozo ya mafunzo ya elimu kwa umma iliyokuwa inatozwa kiasi cha shilingi laki mbili na nusu (250,000/=) kwa kila mshiriki kwa kuwa hili ni jukumu la msingi la OSHA kuelimisha umma.

3. Mabadiliko ya viwango vya ushuru wa forodha;

Kuendelea kutoza kwa mwaka mmoja ushuru wa forodha wa asilimia 35 kwenye mitumba inayoingia kutoka nje (badala ya asilimia 35 au dola za marekani 0.40 kwa kilo moja kutegemea kiwango kipi kikubwa).

4.Mabadiliko ya viwango vya ushuru wa forodha;

Kuendelea kutoza ushuru 35% kwa mwaka mmoja kutoka 100% kwenye sukari ya matumizi ya kawaida (consumption sugar) inayoagizwa kutoka nje ya nchi kwa vibali maalum kwa lengo la kuziba pengo la uzalishaji hapa nchini.

5. Mabadiliko ya viwango vya ushuru wa forodha;

Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwenye ‘Gypsum Powder’ kwa mwaka mmoja.

6. apendekezo ya viwango vya ushuru wa forodha;

Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa 35% badala ya 25% kwenye chokoleti kwa mwaka mmoja, ili kulinda viwanda vya ndani na kukuza ajira.

7 . Kurekebisha Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki Sura 306 ili kuziondoa kampuni zinazomilikiwa na Serikali na ambazo Serikali inamiliki hisa 25% na zaidi katika takwa la kuorodheshwa kwenye soko la hisa, ili kuepusha kupungua kwa hisa za Serikali.

8. Sheria ya Usajili wa Magari

Kufanya marekebisho kwenye sheria hiyo, sura 124, ili kuanzisha usajili wa magari kwa kutumia namba maalum (mfano T. 777 DDD) kwa ada ya 500,000, ili kuwezesha wateja kuchagua namba ya usajili katika namba zilizopo katika regista.

9. Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Serikali za Mitaa apewe mamlaka ya kukusanya tozo ya huduma (Service Levy) 0.3% ya mapato ghafi kwenye sekta ya mawasiliano kwa niaba ya halmashauri, na kuyagawa kwa halmashauri zote ndani ya siku 14 baada ya kukusanywa.

10. Kutokana na athari za kiuchumi zilizosababishwa na #COVID19, serikali imependekeza kutofanya mabadiliko ya viwango maalum vya ushuru wa bidhaa kwa bidhaa zote.

11. Marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato:

Kumpa mamlaka Waziri wa Fedha kutoa msamaha wa Kodi ya Mapato kwenye miradi ya mimkakati yenye kodi ya mapato isiyozidi TZS 1B kwa kipindi chote cha mradi bila kuwasilisha mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad