MTANGAZAJI maarufu Bongo, Zamaradi Mketema, amesema kilichoua sanaa ya Bongo Muvi ni waigizaji wenyewe kwa kutochukulia ‘serious’ kazi hiyo.
Akizungumza kupitia kipindi cha Front Page kinachorushwa na +255GlobalRadio mapema leo Juni 26, 2020 Zamaradi alisema, mbali na kukosekana kwa wasambazaji wakubwa wa filamu, wasanii wenyewe wameshindwa kuwa na umakini katika kazi hiyo na kusababisha soko liyumbe.
“Soko la filamu limeyumba na limeshuka sana na ndiyo maana huwezi kuona soko la DVD kama zamani, watu wamehamia kwenye tamthiliya.
“Makosa si kwa sababu ya kuondoka Kanumba, Kanumba alikuwa aggressive lakini kilichofelisha filamu ni wanafilamu wenyewe,” alisema Zamaradi na kuongeza:
“Makosa yametokana na sisi wenyewe, watu wakawa wamezoea hali. Mtu katoka Iringa, anataka kucheza mwenyewe filamu, na watu wa filamu si kwamba wana njaa bali wanaziendekeza njaa, wanachukua hela na kufanya filamu ambazo hazina ubora.”
Zamaradi amefunguka mengi kupitia +255GlobalRadio unaweza kuisikiliza radio hiyo ya mtandaoni kwa kupakua APP ya Global Publishers lakini pia, unaweza kutazama mahojiano hayo na mengine mengi kupitia Global TV Online inayopatikana YouTube.