Zifahamu Sababu kuu 4 zilizopelekea Maandamano Marekani, Corona yahusishwa


Wakati Donald Trump alipotoa onyo lake , pengine hakufikiria kwamba atalazimika kuishi na hali ngumu kama inayoendeelea nchini Marekani.

Mnamo mwezi Novemba 2014 , huku Marekani ikitishiwa na maandamano makali katika maeneo ya Furguson, Missouri, kutokana na kifo cha kijana Mmarekani mweusi Michael Brown katika mikono ya polisi mzungu Darren Wilson, kilichotokea mwezi Agosti mwaka huo, Trump alitangaza katika Twitter.

‘Taifa letu limevunjika na kutokana na uongozi dhoofu mjini Washington , unaweza kutaraji ghasia na wizi kama vile uliofanyika Furguson kufanyika kwengineko’, aliandika

Miaka mitano na nusu baadaye , huku mitatu akiwa katika uongozi katika jumba la Whitehouse , Marekani inakabiliwa na maandamano mabaya zaidi tangu yale yaliotokea mwaka 1968 baada ya mauaji ya Martin Luther King Jr.

Hali hii imesababishwa na kifo cha George Floyd , Mmarekani mweusi ,46, aliyefariki baada ya afisa wa polisi mzungu kumwekea goti lake katika shingo yake kwa zaidi ya dakika nane.

Ni tukio ambalo linafanana na matukio mengine mengi katika miaka ya hivi karibuni,

Lakini ni kwanini maandamano hayo yamekuwa makubwa zaidi ya yale yaliofanyika Furguson?

Baada ya wiki moja , kumekuwa na maandamano katika zaidi ya miji 75 na kafyu zimewekwa katika zaidi ya miji 40 kati yao.

Maandamano mengi yamesababisha ghasia , makabiliano, wizi na watu kukamatwa.

Licha ya mahitaji ya kutokaribiana ili kuziuia maambukizi ya corona , maandamano hayo yamekuwa makubwaLicha ya mahitaji ya kutokaribiana ili kuziuia maambukizi ya corona , maandamano hayo yamekuwa makubwa
Hali hio imesababisha kutumika kwa jeshi la kitaifa ambalo ,Marekani hulihifadhi tu kwa matukio ya dharurara.

Jeshi hilo siku ya Jumatatu lilipeleka zaidi ya polisi 16,000 katika majimbo 24 na Washington DC.

BBC Mundo inakuelezea sababu zilizopelekea kutokea kwa wimbi hilo la maandamano ambayo hayajawahi kuonekana katika kipindi cha nusu karne.

1. Kifo kilichowaathiri wengi
Tukio la kukamatwa kwa George Floyd ambalo lilisababisha kifo chake baada ya afisa aliyemkamata kumwekea goti katika shingo huku akisema hawezi kupumua , ndio kilichochochea maandamano hayo.

Ukweli ni kwamba kilichosababisha haya yote ni mauaji ya kikatili ya George Floyd wiki iliopita.

‘Mauaji hayo ndio yaliowafanya watu kwenda barabarani na kuandamana’ , alisema Ashley Howard, naibu profesa kuhusu historia ya watu weusi kutoka Chuo kikuu cha Iowa aliyezungumza na BBC

Mtaalamu huyo hatahivyo , anasisitiza kuwa kifo hicho hakikutokea bila sababu, lakini katika msururu wa uchunguzi wa polisi unaofanyiwa watu weusi.

Wakaazi wengi wa Marekani wanaamni kwamba maafisa wa polisi huwanyanyasa Wamarekani weusiWakaazi wengi wa Marekani wanaamni kwamba maafisa wa polisi huwanyanyasa Wamarekani weusi
Hali hii imesababisha dhana ambayo Juliana Zelizer, mtaalamu wa maswala ya siasa ya kihistoria katika chuo kikuu cha Princeton , anaelezea kwamba watu hawa huishi kwa hofu kwasababu wanawaogopa wale wanaohitajika kuwalinda

Ni jambo la kawaiada kupata malalamishi kutoka kwa Wamarekani weusi katika mitandao ya kijamii wakielezea hofu yao ya kuandamwa na polisi kabla ya kukamatwa kwasababu wao ni watu weusi.

Mbali na kwamba wanabaguliwa , kuna data zilizothibitishwa kuonesha kwamba wanasababu za ukweli kuwa na wasiwasi na maafisa wa polisi.

Kiwango cha watu weusi kuuawa na maafisa wa polisi ni mara tatu na nusu zaidi ya kile cha watu weupe kama hawana silaha ama hawajatekeleza shambulio lolote dhidi ya maafisa hao.

Kiwango cha Vijana weusi kuuawa na maafisa wa polisi ni mara 21 zaidi ya vijana weupe kuuawa na maafisa hao.

Maafisa wa polisi huwauawa watu weusi kila baada ya saa 40 , Rashaw Ray, mtafiti katika taasisi ya Brookings, shirika lenye makao yake makuu mjini Washington DC.

M’marekani mweusi mmoja kati 1000 hufariki katika mikono ya polisi. Viwango hivyo vimeimarika kufikia sasa.

Takwimu hizi ndio sababu katika miji ya Minneapolisi, Los Angels , kuna watu wanaandamana na kusababisha ghasia , aliongezea.

Mojawapo ya sababu hizo zimenakiliwa na shirika ambalo lilianzishwa 2013. Watu wengi zaidi wanazidi kuelewa kile kinachotokea, kwamba hili ni tatizo linalopangwa na sio tukio la kipekee.

”Sio tatizo lililopo katika kikosi cha polisi , ni tatizo kubwa ambalo limeendelea kuwepo” , anasema Howard.

2. Ubaguzi
Licha ya hayo yote, utumizi wa nguvu wa kupitia kiasi uliotekelezwa na maafisa wa polisi dhidi yake sio wasiwasi unaowakumba Wamarekani weusi au sababu ya kufanya maandamano.

Wamarekani weusi huwa masikini sana ikilinganishwa na watu weupe nchini humoWamarekani weusi huwa masikini sana ikilinganishwa na watu weupe nchini humo
“Hatuwezi kupuuzilia mbali ukweli kwamba kuna ukosefu mkubwa wa usawa nchini Marekani unaowaathiri Wamarekani weusi.

Hiki ndicho chanzo cha ukosefu wa usawa kati ya maisha ya Wamarekani weusi na watu wa jamii nyingine.

”Tofauti hizo zinaonekana katika mapato na utajiri unaopita kutoka kizazi kimoja hadi chengine, “anasema Howard.

Wataalamu hao pia wanasema idadi ya kuba ya watu weusi hupelekwa jela kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na watu weupe na jamii nyingine mbali na na kwamba kuna tofauti ya elimu wanayopokea watu weusi.

3. Mlipuko virusi vya Corona

Maandamano hayo yanajiri wakati ambapo Marekani imaethirika pakubwa na mlipuko wa virusi vya corona , uliosababisha zaidi ya vifo 100,000 na kuwawacha zaidi ya wafanyakazi milioni 40 bila kazi.

Tunajua kwamba Wamarekani weusi wameathirika pakubwa na ugonjwa huu. Wanaendelea kuambukizwa na kufariki kwa kiwago cha juu ikilinganishwa na raia wengine wa Marekani. Hiyo imenakiliwa.

Wao pia huathirika zaidi kutokana na kazi wanayofanya, kwa mfano ,maafisa wa afya waisaidizi, madereva wa mabasi, makarani na kadhalika,

Kazi zote muhimu hufanywa na watu weusi , suala linalowaweka karibu na maambukizi hayo , anasema Howard.

Wamarekani weusi wameathiriwa pakuba na Covid-19Wamarekani weusi wameathiriwa pakuba na Covid-19
Kulingana na wataalamu wa ugonjwa huo , mlipuko huo umeathiri matatizo yanayowakumba Wamarekani weusi kupitia jinsi watakavyoishi na ugonjwa huo .

Je wanapata matibabu? Je wanaweza kuchukua likizo kazini iwapo ni wagonjwa? Je wanalipwa siku hizo bila kufanya kazi?

Je wana madaktari na mafisa wa afya wanaoweza kuwakimbilia katika jamii ?, Je ni wagonjwa?

Je wanapata usaidizi wa kuwalea watoto wao? Masuala hayo yote ya kibaguzi yanayowakabilia Wamarekani weusi hutumika katika mlipuko kama huu, anasema.

4. Jinsi Ikulu ya Whitehouse ilivyojibu
Zelizer anaelezea kwamba sababu hizi zikichanganywa na jinsi rais Trump alivyolichukulia suala hilo ndizo zilizosababisha ‘moto’ Marekani.

Ili kukabiliana na maandamano hayo wamepeleka na jeshi la kitaifa kuwakabilia waandamanajiIli kukabiliana na maandamano hayo wamepeleka na jeshi la kitaifa kuwakabilia waandamanaji
Kuna hatua tofauti ambazo Trump angechukua anapokabiliwa na hali kama hii, lakini kwa jumla, jibu lake lilikuwa kusababisha ghasia dhidi ya waandamanaji, anasema

Mtaalamu huyo anahoji wito wa rais wa kuwalazimisha watu kufuata sheria akisema Trump alisema kwamba: Wizi utavutia ufyatuaji wa risasi sawa na wito uliotolewa miongo kadhaa iliopita. Watu wanahitaji rais anayetoa wito wa utulivu na ambae anasikiliza na kuchukua hatua dhidi ya chanzo cha yanayotokea”, alisema Zelizer.

”Trump hajachukua hatua kama hizo”, anamaliza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad