Afisa wa WHO anasema AIDS kama muongozo wa kupambana na corona
0
July 11, 2020
Mifumo ya afya duniani inahitajika kuendelezwa ili kudhibiti maambukizo ya magonjwa na kuweza kuwahudumia idadi kubwa ya wagonjwa katika wakati huu wa janga la virusi vya corona pamoja na majanga mengine yanayoweza kuzuka hapo baadae, mkuu wa mpango wa dharura wa shirika la afya ulimwenguni WHO ameonya jana.
Dr. Michael Ryan wa WHO, akizungumza katika kikao kilichotayarishwa na chama cha kimataifa kinachohusika na ugonjwa wa ukimwi kwa njia ya vidio, amesema viongozi wa dunia wakipambana na janga lililopo hivi sasa, wanapaswa kujifunza kutoka kwa wanaharakati wa ugonjwa wa HIV na ukimwi, na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya afya unawezekana na ulipo katika msingi wa ushahidi.
Janga la virusi vya corona , ambalo bado halijafikia kiwango cha juu katika sehemu nyingi za dunia, limeweka wazi mapungufu na kusababisha mabilioni ya watu kutokuwa na uwezo wa kupata huduma ya kutumainika na rahisi ya afya.
Tags