Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga, amesema kitendo Hayati Benjamin Mkapa kukiri mambo aliyowahi kukosea wakati wa uongozi wake akiwa Mkuu wa nchi katika kitabu chake cha ‘My life My Purpose’ ni ishara ya unyenyekevu na kumpenda Mungu.
Askofu Nyaisonga, ametoa kauli hiyo leo wakati wa ibada ya mazishi ya kuaga mwili wa Hayati Mkapa katika jijini cha Lupaso na kuwataka watu kuishi maisha ya haki, utu na uadilifu ili kusudio la Mungu katika uumbaji lipate kutimia, kwa kuwa tulipo ni wasafiri na kwamba inatupasa kuishi na kutenda kwa busara mema tusije tukalemewa na kubeza tunayaona, na tutumie vizuri muda wa sasa.
“Kama mnavyoona alifanya toba ya hadhara na kuandika kitabu chake cha ‘My Life My Purpose’ toba ni hujenga, uvumilivu, msamaha, kujikatalia, uwajibikaji na nyingine nyingi ambazo zimebaki kama kielelezo cha kufikia uzima wa milelealisisitiza
Moja ya mambo aliyokiri kukosea katika kitabu chake hicho ni kuhusiana na suala la Jeshi la Polisi kuwavamia na kuwapiga wafuasi wa upinzani walipokuwa wakiandamana mwaka 2001 visiwani Zanzibar jambo lililosababisha mauaji jambo ambalo halikumfurahisha yeye wakati akiwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema dhambi ya kutofanya kitu ndiyo inatawala dunia kwa leo, hutashitakiwa na mtu lakini hutashtakiwa kwa kutofanya lolote, na kwamba siyo kuungama kwa maneno bali kutafsiri kwa vitendo na kwadhati tunayojifunza.
Askofu Nyaisonga, amesema Rais Mkapa kila alipokwenda kusoma ndani na nje ya nchi alijiunga na chama cha wanafunzi Wakotoliki, jambo ambalo ni fundisho kwa watu na kwamba hakuogopwa na watu ndani na nje ya kanisa, na hakuogopwa na watu wake .