Baada ya Kukosa Ubingwa Hizi hapa Hesabu za Yanga


KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Ubelgiji, Luc Eymael amefunguka kuwa kitu pekee kilichobaki katika mikono yao ni kuhakikisha kuwa wanaitwaa nafasi ya pili kwenye ligi kuu ili kuipa heshima timu hiyo.

Eymael amesema hawawezi kumaliza ligi wakiwa wamekosa kila kitu, hivyo kumaliza wakiwa katika nafasi ya pili ndiyo mafanikio pekee kwao kwa msimu huu na watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hawaikosi nafasi hiyo ili kuiepusha Yanga na aibu.

Kesho, Julai 22, Yanga itakuwa kazini kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi ambao utachezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Tayari bingwa ashajulikana na amekabidhiwa ubingwa wake ambaye ni Simba mwenye pointi 84 kibindoni kwa sasa ndani ya ligi huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 66 zote zimecheza mechi 36.

Eymael amesema:"Hakuna namna nyingine ambayo tunaweza kufanya kwa sasa zaidi ya kupambana kumaliza ligi tukiwa nafasi ya pili.

"Tumekosa ubingwa na tumepoteza nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kupitia Kombe la Shirikisho huku tutapambana kufikia malengo yetu hamna namna."

Pia Yanga iliyeyusha nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa mabao 4-1 na Simba kwenye mchezo wa robo fainali jambo lililowafanya wasiwe na tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Vita yao kwenye nafasi ya pili ni dhidi ya Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu kibindoni ina pointi 66 baada ya kucheza mechi 36.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad