Baba Mkwe na Mama Mkwe Wanataka Kunimaliza ili Mtoto wao Arithi Mali zangu

Kiufupi nimeoa mwaka 2017 na tumejaaliwa mtoto mmoja, ila kuanzia mwezi wa 12 mwaka jana nimekuwa katika hali ngumu na mke wangu katika ndoa, amekuwa hanisikii mimi kama mmewe kila kitu anaendeshwa na wazazi wake .

Sasa imefikia baba yake kumuambia adai talaka arudi nyumbani, nilipojua hiyo njama nikawahusisha wazee wa pande zote mbili ,ila kule kwao wakakataa kuhusika, siku sio chache mke wangu akanishitaki kwenye baraza la wazee kuwa anataka haki yake amechoka kuishi na mimi. Nikaitwa kwenye kikao cha wajumbe, akaulizwa aseme shida yake nini , akajibu kuwa anataka tugawe mali zote kila mtu ajue maisha yake, akaulizwa hizo mali mmechuma na mmeo au ulizikuta? Akajibu nimezikuta.

Akaulizwa ni mali gani mmechuma na mmeo tokea mmeoana? Akajibu hatukacha mali yoyote. Wajumbe wakamjibu kuwa kulingana na alikuta hizo mali zote basi hizo mali hazikuhusu.

Tokea hapo alibadili upepo akawa mtulivu hata ile hali ikaisha, sasa kumbe ile hali ilibadilishwa upepo na kuelekezwa kwa ushirikina, ushahidi niliupata kutoka kwa mtu wa karibu na mama mkwe wangu( mama wa mke wangu) kuwa mama mkwe wako anakuendea kwa waganga akuue mwanae arithi hizo mali.

Sasa kwa haya mafupi naombeni maoni na ushauri.

Nawasilisha!
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad